Exodus 3:18 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“Wao watakusikiliza, nawe pamoja na wazee wa Waisraeli mtamwendea mfalme wa Misri na kumwambia, ‘Mwenyezi-Mungu, Mungu wa Waebrania, ametutokea. Sasa, uturuhusu tuende safari ya mwendo wa siku tatu jangwani, tukamtambikie Mwenyezi-Mungu, Mungu wetu.’
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Wazee wa Israeli watakusikiliza. Kisha wewe na wazee mtaenda kwa mfalme wa Misri na kumwambia, ‘Mwenyezi Mungu, Mungu wa Waebrania, ametutokea. Turuhusu twende safari ya siku tatu huko jangwani kutoa dhabihu kwa Mwenyezi Mungu, Mungu wetu.’
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Nao watakusikia sauti yako; nawe utakwenda, wewe na wazee wa Israeli kwa mfalme wa Misri, na kumwambia, Bwana Mungu wa Waebrania, amekutana nasi; basi sasa twakuomba, tupe ruhusa twende mwendo siku tatu jangwani, ili tumtolee dhabihu Bwana Mungu wetu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“Wao watakusikiliza, nawe pamoja na wazee wa Waisraeli mtamwendea mfalme wa Misri na kumwambia, ‘Mwenyezi-Mungu, Mungu wa Waebrania, ametutokea. Sasa, uturuhusu tuende safari ya mwendo wa siku tatu jangwani, tukamtambikie Mwenyezi-Mungu, Mungu wetu.’
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Wazee wa Israeli watakusikiliza. Kisha wewe na wazee mtakwenda kwa mfalme wa Misri na kumwambia, ‘BWANA, Mungu wa Waebrania ametutokea. Turuhusu tuende safari ya siku tatu huko jangwani kutoa dhabihu kwa BWANA Mungu wetu.’
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Wazee wa Israeli watakusikiliza. Kisha wewe na wazee mtakwenda kwa mfalme wa Misri na kumwambia, ‘ bwana, Mungu wa Waebrania ametutokea. Turuhusu twende safari ya siku tatu huko jangwani kutoa dhabihu kwa bwana Mwenyezi Mungu wetu.’
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Nao watakusikia sauti yako; nawe utakwenda, wewe na wazee wa Israeli kwa mfalme wa Misri, na kumwambia, BWANA Mungu wa Waebrania, amekutana nasi; basi sasa twakuomba, tupe ruhusa twende mwendo wa siku tatu jangwani, ili tumtolee dhabihu BWANA Mungu wetu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
“Wao watakusikiliza, nawe pamoja na wazee wa Waisraeli mtamwendea mfalme wa Misri na kumwambia, ‘Mwenyezi-Mungu, Mungu wa Waebrania, ametutokea. Sasa, uturuhusu tuende safari ya mwendo wa siku tatu jangwani, tukamtambikie Mwenyezi-Mungu, Mungu wetu.’
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Watakapoisikia sauti yako, utakwenda wewe pamoja na wazee wa Waisiraeli kwa mfalme wa Misri, umwambie: Bwana Mungu wa Waebureo amekutana nasi; kwa hiyo sasa tunataka kwenda nyikani safari ya siku tatu, tumtambikie Bwana Mungu wetu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Nao watakusikia sauti yako; nawe utakwenda, wewe na wazee wa Israeli kwa mfalme wa Misri, na kumwambia, BWANA Mungu wa Waebrania, amekutana nasi; basi sasa twakuomba, tupe ruhusa twende mwendo siku tatu jangwani, ili tumtolee dhabihu BWANA Mungu wetu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
“Wao watakusikiliza, nawe pamoja na wazee wa Waisraeli mutamwendea mufalme wa Misri na kumwambia: ‘Yawe, Mungu wa Waebrania, ametutokea. Sasa, uturuhusu tuende safari ya mwendo wa siku tatu katika jangwa, tumutolee Yawe, Mungu wetu, sadaka.’