Exodus 3:2 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Basi, malaika wa Mwenyezi-Mungu akamtokea katika mwali wa moto katikati ya kichaka. Mose akaangalia, akashangaa kuona kichaka kinawaka moto na wala hakiungui.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Huko malaika wa Mwenyezi Mungu akamtokea Musa katika mwali wa moto kutoka kichakani. Musa akaona kwamba ingawa kile kichaka kilikuwa kinawaka moto, kilikuwa hakiteketei.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Malaika wa Bwana akamtokea, katika mwali wa moto uliotoka katikati ya kijiti; akatazama, na kumbe! Kile kijiti kiliwaka moto, nacho kijiti hakikuteketea.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Basi, malaika wa Mwenyezi-Mungu akamtokea katika mwali wa moto katikati ya kichaka. Mose akaangalia, akashangaa kuona kichaka kinawaka moto na wala hakiungui.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Huko malaika wa BWANA akamtokea Mose katika mwali wa moto kutoka katika kichaka. Mose akaona hilo, ingawa kile kichaka kilikuwa kinawaka moto, kilikuwa hakiteketei.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Huko malaika wa bwana akamtokea Musa katika mwali wa moto kutoka kichakani. Musa akaona kwamba ingawa kile kichaka kilikuwa kinawaka moto, kilikuwa hakiteketei.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Malaika wa BWANA akamtokea, katika mwali wa moto uliotoka katikati ya kichaka; akatazama, na kumbe! Kile kichaka kiliwaka moto, nacho kichaka hakikuteketea.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Basi, malaika wa Mwenyezi-Mungu akamtokea katika mwali wa moto katikati ya kichaka. Mose akaangalia, akashangaa kuona kichaka kinawaka moto na wala hakiungui.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ndipo, malaika wa Bwana alipomtokea katika moto uliowaka kichakani katikati; naye alipotazama akaona: Kichaka hiki kinawaka moto kweli, lakini kichaka hiki hakiungui.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Malaika wa BWANA akamtokea, katika mwali wa moto uliotoka katikati ya kijiti; akatazama, na kumbe! Kile kijiti kiliwaka moto, nacho kijiti hakikuteketea.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Basi, malaika wa Yawe akamutokea katika mwali wa moto katikati ya kichaka. Musa akaangalia, akashangaa kuona kichaka kinawaka moto na wala hakiungui.