Exodus 30:16 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Wewe utaipokea fedha hiyo ya upatanisho kutoka kwa Waisraeli, nawe utaitumia kwa shughuli za kazi za hema takatifu, nayo iwe ni ukumbusho wa Waisraeli mbele yangu, fidia ya maisha yenu.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Utapokea fedha ya upatanisho kutoka kwa Waisraeli na uzitumie kwa ajili ya huduma ya Hema la Kukutania. Itakuwa ni ukumbusho kwa Waisraeli mbele za Mwenyezi Mungu kufanya upatanisho kwa ajili ya nafsi zenu.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Nawe utapokea hizo fedha za upatanisho mikononi mwa hao wana wa Israeli, na kuziweka kwa ajili ya utumishi wa hema ya kukutania; ili kwamba ziwe ukumbusho kwa ajili ya wana wa Israeli mbele ya Bwana, ili kufanya upatanisho kwa ajili ya roho zenu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Wewe utaipokea fedha hiyo ya upatanisho kutoka kwa Waisraeli, nawe utaitumia kwa shughuli za kazi za hema takatifu, nayo iwe ni ukumbusho wa Waisraeli mbele yangu, fidia ya maisha yenu.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Utapokea fedha ya upatanisho kutoka kwa Waisraeli na uzitumie kwa ajili ya huduma ya Hema la Kukutania. Itakuwa ni ukumbusho kwa Waisraeli mbele za BWANA kufanya upatanisho kwa ajili ya nafsi zenu.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Utapokea fedha ya upatanisho kutoka kwa Waisraeli na uzitumie kwa ajili ya huduma ya Hema la Kukutania. Itakuwa ni ukumbusho kwa Waisraeli mbele za bwana kufanya upatanisho kwa ajili ya nafsi zenu.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Nawe utapokea hizo fedha za upatanisho mikononi mwa hao wana wa Israeli, na kuziweka kwa ajili ya utumishi wa hema ya kukutania; ili kwamba ziwe ukumbusho kwa ajili ya wana wa Israeli mbele za BWANA, ili kufanya upatanisho kwa ajili ya roho zenu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Wewe utaipokea fedha hiyo ya upatanisho kutoka kwa Waisraeli, nawe utaitumia kwa shughuli za kazi za hema takatifu, nayo iwe ni ukumbusho wa Waisraeli mbele yangu, fidia ya maisha yenu.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kisha uzichukue hizo fedha za mapoza, utakazowatoza wana wa Isiraeli, uzitumie za utumishi wa hema la Mkutano; ndivyo, zitakavyokuwa za kumkumbusha Bwana, awakumbuke wana wa Isiraeli, azipatie roho zenu upozi.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Nawe utapokea hizo fedha za upatanisho mikononi mwa hao wana wa Israeli, na kuziweka kwa ajili ya utumishi wa hema ya kukutania; ili kwamba ziwe ukumbusho kwa ajili ya wana wa Israeli mbele ya BWANA, ili kufanya upatanisho kwa ajili ya roho zenu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Wewe utaipokea feza hiyo ya upatanisho kutoka kwa Waisraeli, nawe utaitumia kwa shuguli za kazi za hema takatifu, nayo ikuwe ni ukumbusho wa Waisraeli mbele yangu, malipo ya maisha yenu.