Exodus 31:13 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“Waambie Waisraeli hivi: Nyinyi mtaadhimisha Sabato zangu, kwa sababu hizo ni ishara kati yenu na mimi kwa vizazi vyote kwamba mimi ndimi ninayewatakasa.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Waambie Waisraeli, ‘Ninyi ni lazima mzishike Sabato zangu. Hii itakuwa ni ishara kati yangu na ninyi kwa vizazi vijavyo, ili mpate kujua kwamba Mimi Ndimi Mwenyezi Mungu, niwafanyaye ninyi watakatifu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kisha, nena wewe na wana wa Israeli, na kuwaambia, Hakika mtazishika Sabato zangu, kwa kuwa ni ishara kati ya mimi na ninyi katika vizazi vyenu vyote; ili mpate kujua ya kuwa mimi ndimi Bwana niwatakasaye ninyi.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“Waambie Waisraeli hivi: Nyinyi mtaadhimisha Sabato zangu, kwa sababu hizo ni ishara kati yenu na mimi kwa vizazi vyote kwamba mimi ndimi ninayewatakasa.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Waambie Waisraeli, ‘Ninyi ni lazima mzishike Sabato zangu. Hii itakuwa ni ishara kati yangu na ninyi kwa ajili ya vizazi vijavyo, ili mpate kujua kwamba Mimi Ndimi BWANA, niwafanyaye ninyi watakatifu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Waambie Waisraeli, ‘Ninyi ni lazima mzishike Sabato zangu. Hii itakuwa ni ishara kati yangu na ninyi kwa ajili ya vizazi vijavyo, ili mpate kujua kwamba Mimi Ndimi bwana, niwafanyaye ninyi watakatifu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kisha, nena na wana wa Israeli, na kuwaambia, Hakika mtazishika Sabato zangu, kwa kuwa ni ishara kati yenu na mimi katika vizazi vyenu vyote; ili mpate kujua ya kuwa mimi ndimi BWANA niwatakasaye ninyi.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
“Waambie Waisraeli hivi: Nyinyi mtaadhimisha Sabato zangu, kwa sababu hizo ni ishara kati yenu na mimi kwa vizazi vyote kwamba mimi ndimi ninayewatakasa.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Wewe sema na wana wa Isiraeli na kuwaambia: Ziangalieni siku zangu za mapumziko, ziwe kielekezo cha Agano, nililoliagana nanyi, wao wa vizazi vyenu vijavyo wajue, ya kuwa mimi Bwana ndimi mwenye kuwatakasa ninyi.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kisha, nena wewe na wana wa Israeli, na kuwaambia, Hakika mtazishika Sabato zangu, kwa kuwa ni ishara kati ya mimi na ninyi katika vizazi vyenu vyote; ili mpate kujua ya kuwa mimi ndimi BWANA niwatakasaye ninyi.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Uwaambie Waisraeli hivi: Ninyi mutashika hakika Sabato zangu, kwa sababu hizo ni kitambulisho kati yenu na mimi kwa vizazi vyote kwamba mimi ndimi ninayewatakasa.