Exodus 31:14 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mtaiadhimisha Sabato, nayo itakuwa kwenu siku takatifu. Yeyote atakayeitia unajisi siku hiyo lazima auawe. Na mtu atakayefanya kazi yoyote siku hiyo atatengwa mbali na watu wake.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“ ‘Mtaishika Sabato, kwa sababu ni takatifu kwenu. Yeyote atakayeinajisi lazima auawe, yeyote atakayefanya kazi siku hiyo lazima akatiliwe mbali na watu wake.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi mtaishika hiyo Sabato; kwa kuwa ni takatifu kwenu; kila mtu atakayeitia unajisi hakika yake atauawa; kwa kuwa kila mtu afanyaye kazi katika siku hiyo, nafsi hiyo itakatiliwa mbali na watu wake.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mtaiadhimisha Sabato, nayo itakuwa kwenu siku takatifu. Yeyote atakayeitia unajisi siku hiyo lazima auawe. Na mtu atakayefanya kazi yoyote siku hiyo atatengwa mbali na watu wake.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“ ‘Mtaishika Sabato, kwa sababu ni takatifu kwenu. Ye yote atakayeinajisi lazima auawe, ye yote atakayefanya kazi siku hiyo lazima akafie mbali na watu wake.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“ ‘Mtaishika Sabato, kwa sababu ni takatifu kwenu. Yeyote atakayeinajisi lazima auawe, yeyote atakayefanya kazi siku hiyo lazima akafie mbali na watu wake.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi mtaishika hiyo Sabato; kwa kuwa ni takatifu kwenu; kila mtu atakayeitia unajisi hana budi atauawa; na kila mtu afanyaye kazi siku hiyo, ataondolewa toka kwa watu wake.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mtaiadhimisha Sabato, nayo itakuwa kwenu siku takatifu. Yeyote atakayeitia unajisi siku hiyo lazima auawe. Na mtu atakayefanya kazi yoyote siku hiyo atatengwa mbali na watu wake.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwa hiyo iangalieni siku ya mapumziko, ipate kuwa takatifu kwenu. Atakayelivunja hili agizo la kuitakasa hana budi kufa, kwani kila atakayefanya kazi siku hiyo, roho yake sharti ing'olewe kwao walio wa ukoo wake.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi mtaishika hiyo Sabato; kwa kuwa ni takatifu kwenu; kila mtu atakayeitia unajisi hakika yake atauawa; kwa kuwa kila mtu afanyaye kazi katika siku hiyo, nafsi hiyo itakatiliwa mbali na watu wake.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mutashika Sabato, nayo itakuwa kwenu siku takatifu. Yeyote atakayeichafua siku hiyo anapaswa kuuawa. Na mutu atakayefanya kazi yoyote siku hiyo atatengwa mbali na watu wake.