Exodus 32:1 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Watu walipoona kuwa Mose amechelewa kurudi kutoka mlimani, walikusanyika mbele ya Aroni na kumwambia, “Haya! Tutengenezee miungu itakayotuongoza maana hatujui lililompata huyo Mose aliyetutoa nchini Misri.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Watu walipoona kuwa Musa amekawia sana kushuka kutoka mlimani, walimsonga Haruni na kumwambia, “Njoo, tutengenezee miungu itakayotutangulia. Kwa maana huyu jamaa yetu Musa aliyetupandisha kutoka Misri, hatujui yaliyompata.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Hata watu walipoona ya kuwa Musa amekawia kushuka katika mlima, wakakusanyana wakamwendea Haruni, wakamwambia, Haya! Katufanyizie miungu itakayokwenda mbele yetu, kwa maana Musa huyo aliyetutoa katika nchi ya Misri hatujui yaliyompata.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Watu walipoona kuwa Mose amechelewa kurudi kutoka mlimani, walikusanyika mbele ya Aroni na kumwambia, “Haya! Tutengenezee miungu itakayotuongoza maana hatujui lililompata huyo Mose aliyetutoa nchini Misri.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Watu walipoona kuwa Mose amekawia sana kushuka kutoka mlimani, walimkusanyikia Aroni na kumwambia, “Njoo, tutengenezee miungu itakayotutangulia. Kwa maana huyu jamaa yetu Mose aliyetupandisha kutoka Misri, hatujui jambo lililompata.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Watu walipoona kuwa Musa amekawia sana kushuka kutoka mlimani, walimkusanyikia Haruni na kumwambia, “Njoo, tutengenezee miungu itakayotutangulia. Kwa maana huyu jamaa yetu Musa aliyetupandisha kutoka Misri, hatujui jambo lililompata.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Hata watu walipoona ya kuwa Musa amekawia kushuka katika mlima, wakakusanyana wakamwendea Haruni, wakamwambia, Haya! Katufanyizie miungu itakayokwenda mbele yetu, kwa maana Musa huyo aliyetutoa katika nchi ya Misri hatujui yaliyompata.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Watu walipoona kuwa Mose amechelewa kurudi kutoka mlimani, walikusanyika mbele ya Aroni na kumwambia, “Haya! Tutengenezee miungu itakayotuongoza maana hatujui lililompata huyo Mose aliyetutoa nchini Misri.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Watu walipoona, ya kuwa Mose anakawia kushuka mlimani, watu wakamkusanyikia Haroni, wakamwambia: Haya! Tufanyie miungu itakayotuongoza! Kwani hatuyajui yaliyompata huyo Mose aliyetutoa katika nchi ya Misri.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Hata watu walipoona ya kuwa Musa amekawia kushuka katika mlima, wakakusanyana wakamwendea Haruni, wakamwambia, Haya! Katufanyizie miungu itakayokwenda mbele yetu, kwa maana Musa huyo aliyetutoa katika nchi ya Misri hatujui yaliyompata.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Watu walipoona kwamba Musa amechelewa kurudi kutoka juu ya mulima, wakakusanyika mbele ya Haruni na kumwambia: Basi! Ututengenezee miungu itakayotuongoza, maana hatujui jambo lililomupata yule Musa aliyetutoa katika inchi ya Misri.