Exodus 32:11 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Lakini Mose akamsihi Mwenyezi-Mungu, Mungu wake, akisema, “Ee Mwenyezi-Mungu, kwa nini hasira yako inawaka vikali dhidi ya watu wako uliowatoa nchini Misri kwa uwezo mkuu na mkono wenye nguvu?
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Lakini Musa akamsihi Mwenyezi Mungu, Mungu wake, akasema, “Ee Mwenyezi Mungu, kwa nini hasira yako iwake dhidi ya watu wako, wale uliowatoa Misri kwa uweza mkuu na mkono wenye nguvu?
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Musa akamsihi sana Bwana, Mungu wake, na kusema, Bwana, kwa nini hasira zako kuwaka juu ya watu wako uliowaleta kutoka nchi ya Misri kwa uweza mkuu, na kwa mkono wenye nguvu?
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Lakini Mose akamsihi Mwenyezi-Mungu, Mungu wake, akisema, “Ee Mwenyezi-Mungu, kwa nini hasira yako inawaka vikali dhidi ya watu wako uliowatoa nchini Misri kwa uwezo mkuu na mkono wenye nguvu?
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Lakini Mose akamsihi BWANA Mungu wake, akasema, “Ee BWANA, kwa nini hasira yako iwake dhidi ya watu wako, wale uliowatoa Misri kwa uweza mkuu na mkono wenye nguvu?
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Lakini Musa akamsihi bwana Mwenyezi Mungu wake, akasema, “Ee bwana, kwa nini hasira yako iwake dhidi ya watu wako, wale uliowatoa Misri kwa uweza mkuu na mkono wenye nguvu?
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Musa akamsihi sana BWANA, Mungu wake, na kusema, BWANA, kwa nini hasira zako kuwaka juu ya watu wako uliowaleta kutoka nchi ya Misri kwa uweza mkuu, na kwa mkono wenye nguvu?
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Lakini Mose akamsihi Mwenyezi-Mungu, Mungu wake, akisema, “Ee Mwenyezi-Mungu, kwa nini hasira yako inawaka vikali dhidi ya watu wako uliowatoa nchini Misri kwa uwezo mkuu na mkono wenye nguvu?
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini Mose akambembeleza Bwana Mungu wake kwamba: Bwana, mbona utayaacha makali yako, yawawakie watu wako, uliowatoa katika nchi ya Misri kwa uwezo mkuu na kwa mkono ulio na nguvu?
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Musa akamsihi sana BWANA, Mungu wake, na kusema, BWANA, kwa nini hasira zako kuwaka juu ya watu wako uliowaleta kutoka nchi ya Misri kwa uweza mkuu, na kwa mkono wenye nguvu?
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Lakini Musa akamusihi Yawe, Mungu wake, akisema: Ee Yawe, kwa nini hasira yako inawaka vikali juu ya watu wako uliowatoa katika inchi ya Misri kwa uwezo mukubwa na mukono wenye nguvu?