Exodus 32:12 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Ukifanya hivyo, hakika Wamisri watasema, ‘Aliwatoa kwa nia mbaya ili kuwaulia mlimani na kuwateketeza kabisa duniani.’ Ee Mwenyezi-Mungu, tuliza hasira yako kali na kuacha jambo hilo baya ulilokusudia kufanya dhidi ya watu wako.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kwa nini Wamisri waseme, ‘Ni kwa nia mbaya aliwatoa Misri, ili awaue milimani na kuwafuta usoni mwa dunia’? Achilia mbali hasira yako kali, waonee huruma na usilete maafa juu ya watu wako.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kwa nini Wamisri kunena, wakisema, Amewatoa kwa kuwatenda uovu, ili apate kuwaua milimani, na kuwaondoa watoke juu ya uso wa nchi? Geuka katika hasira yako kali, ughairi uovu huu ulio nao juu ya watu wako.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Ukifanya hivyo, hakika Wamisri watasema, ‘Aliwatoa kwa nia mbaya ili kuwaulia mlimani na kuwateketeza kabisa duniani.’ Ee Mwenyezi-Mungu, tuliza hasira yako kali na kuacha jambo hilo baya ulilokusudia kufanya dhidi ya watu wako.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kwa nini Wamisri waseme, ‘Ni kwa nia mbaya aliwatoa Misri, ili awaue milimani na kuwafuta usoni mwa dunia’? Achilia mbali hasira yako kali, waonee huruma na usilete maafa juu ya watu wako.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kwa nini Wamisri waseme, ‘Ni kwa nia mbaya aliwatoa Misri, ili awaue milimani na kuwafuta usoni mwa dunia’? Achilia mbali hasira yako kali, waonee huruma na usilete maafa juu ya watu wako.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kwa nini Wamisri waseme, kuwa “Amewatoa ili awatende mabaya, apate kuwaua milimani na kuwaangamiza watoke juu ya uso wa nchi?” Geuka katika hasira yako kali, ughairi uovu huu ulio nao juu ya watu wako.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Ukifanya hivyo, hakika Wamisri watasema, ‘Aliwatoa kwa nia mbaya ili kuwaulia mlimani na kuwateketeza kabisa duniani.’ Ee Mwenyezi-Mungu, tuliza hasira yako kali na kuacha jambo hilo baya ulilokusudia kufanya dhidi ya watu wako.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Mbona unataka, Wamisri waseme kwamba: Aliwatoa kwa ubaya, awaue milimani na kuwatowesha juu ya nchi? Geuka na kuyaacha makali yako yanayowaka moto, uwahurumie walio ukoo wako kwa ajili ya mabaya, waliyoyafanya!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kwa nini Wamisri kunena, wakisema, Amewatoa kwa kuwatenda uovu, ili apate kuwaua milimani, na kuwaondoa watoke juu ya uso wa nchi? Geuka katika hasira yako kali, ughairi uovu huu ulio nao juu ya watu wako.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Ukifanya hivyo, hakika Wamisri watasema: Aliwatoa kwa nia mbaya kwa kuwaua kwenye mulima na kuwateketeza kabisa katika dunia. Ee Yawe, tuliza hasira yako kali na kuacha jambo hilo baya ulilokusudia kufanya juu ya watu wako.