Exodus 32:27 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Akawaambia, “Mwenyezi-Mungu, Mungu wa Israeli, anasema hivi: ‘Kila mtu na ajifunge upanga wake kiunoni, azunguke kila mahali kambini, kutoka lango moja hadi lingine, na kila mmoja amuue ndugu yake, rafiki yake na jirani yake.’”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ndipo alipowaambia, “Hili ndilo Mwenyezi Mungu, Mungu wa Israeli, asemalo: ‘Kila mmoja wenu ajifunge upanga wake kiunoni aende huku na huko kambi yote mwisho hadi mwisho mwingine, kila mmoja amuue ndugu yake, na rafiki yake na jirani yake.’ ”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Akawaambia, Bwana, Mungu wa Israeli, asema hivi, Kila mtu na ajifunge upanga wake pajani mwake, akapite huko na huko toka mlango hata mlango kati ya marago, mkamchinje kila mtu ndugu yake, na kila mtu mwenziwe na kila mtu jirani yake.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Akawaambia, “Mwenyezi-Mungu, Mungu wa Israeli, anasema hivi: ‘Kila mtu na ajifunge upanga wake kiunoni, azunguke kila mahali kambini, kutoka lango moja hadi lingine, na kila mmoja amuue ndugu yake, rafiki yake na jirani yake.’”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ndipo alipowaambia, “Hili ndilo BWANA, Mungu wa Israeli asemalo: ‘Kila mmoja wenu ajifunge upanga wake kiunoni aende huku na huko kambi yote mwisho hadi mwisho mwingine, kila mmoja amuue ndugu yake, na rafiki yake na jirani yake.’ ”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ndipo alipowaambia, “Hili ndilo bwana, Mungu wa Israeli asemalo: ‘Kila mmoja wenu ajifunge upanga wake kiunoni aende huku na huko kambi yote mwisho hadi mwisho mwingine, kila mmoja amuue ndugu yake, na rafiki yake na jirani yake.’ ”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Akawaambia, BWANA, Mungu wa Israeli, asema hivi, Kila mtu na ajifunge upanga wake pajani mwake, akapite huku na huko toka mlango hata mlango kati ya kambi, mkamchinje kila mtu ndugu yake, na kila mtu mwenziwe na kila mtu jirani yake.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Akawaambia, “Mwenyezi-Mungu, Mungu wa Israeli, anasema hivi: ‘Kila mtu na ajifunge upanga wake kiunoni, azunguke kila mahali kambini, kutoka lango moja hadi lingine, na kila mmoja amuue ndugu yake, rafiki yake na jirani yake.’”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
akawaambia: Hivi ndivyo, alivyosema Bwana Mungu wa Isiraeli: Jifungeni kila mtu upanga wake kiunoni pake, mzunguke makambini kwenda na kurudi toka lango la huku hata lango la huko, mkiua kila mtu ndugu yake naye mwenzake naye rafiki yake!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Akawaambia, BWANA, Mungu wa Israeli, asema hivi, Kila mtu na ajifunge upanga wake pajani mwake, akapite huko na huko toka mlango hata mlango kati ya marago, mkamchinje kila mtu ndugu yake, na kila mtu mwenziwe na kila mtu jirani yake.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Akawaambia: Yawe, Mungu wa Israeli, anasema hivi: Kila mutu ajifungie upanga wake kwenye kiuno, azunguke kila pahali katika kambi, kutoka mulango moja mpaka mwingine, na kila mumoja amwue ndugu yake, rafiki yake na jirani yake.