Exodus 32:29 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mose akasema, “Leo mmejiweka wakfu nyinyi wenyewe kumhudumia Mwenyezi-Mungu, kwa vile hamkusita hata kuwaua watoto wenu au ndugu zenu. Mungu awajalie baraka leo hii.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kisha Musa akasema, “Leo mmewekwa wakfu kwa Mwenyezi Mungu, kwa kuwa mlikuwa kinyume na wana wenu wenyewe na ndugu zenu, naye Mungu amewabariki leo.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Musa akasema, Jiwekeni wakfu kwa Bwana leo, naam, kila mtu juu ya mwanawe na juu ya ndugu yake; ili awape baraka leo.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mose akasema, “Leo mmejiweka wakfu nyinyi wenyewe kumhudumia Mwenyezi-Mungu, kwa vile hamkusita hata kuwaua watoto wenu au ndugu zenu. Mungu awajalie baraka leo hii.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kisha Mose akasema, “Leo mmewekwa wakfu kwa BWANA, kwa kuwa mlikuwa kinyume na wana wenu wenyewe na ndugu zenu, naye Mungu amewabariki leo.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kisha Musa akasema, “Leo mmewekwa wakfu kwa bwana, kwa kuwa mlikuwa kinyume na wana wenu wenyewe na ndugu zenu, naye Mungu amewabariki leo.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Musa akasema, Jiwekeni wakfu kwa BWANA leo, kila mtu juu ya mwanawe na juu ya ndugu yake; ili awape baraka leo.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mose akasema, “Leo mmejiweka wakfu nyinyi wenyewe kumhudumia Mwenyezi-Mungu, kwa vile hamkusita hata kuwaua watoto wenu au ndugu zenu. Mungu awajalie baraka leo hii.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kisha Mose akawaambia: Yajazeni leo magao yenu, mwe wa Bwana, maana kila mmoja wenu hakumjua wala mtoto wake wala ndugu yake; Bwana na awape leo mbaraka!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Musa akasema, Jiwekeni wakfu kwa BWANA leo, naam, kila mtu juu ya mwanawe na juu ya ndugu yake; ili awape baraka leo.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Musa akasema: Leo mumejitakasa ninyi wenyewe kwa kumutumikia Yawe, kwa vile hamukusita hata kuwaua watoto wenu au wandugu zenu. Mungu awajalie baraka leo hii.