Exodus 32:35 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mwenyezi-Mungu akawapelekea watu ugonjwa wa tauni, kwa kuwa walimwomba Aroni awafanyie yule ndama wa dhahabu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ndipo Mwenyezi Mungu akawapiga watu kwa ugonjwa wa tauni kwa sababu ya yale waliyoyafanya na ndama yule ambaye alitengenezwa na Haruni.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Bwana akawapiga hao watu, kwa walivyoifanya ile ndama, ambayo Haruni aliifanya.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mwenyezi-Mungu akawapelekea watu ugonjwa wa tauni, kwa kuwa walimwomba Aroni awafanyie yule ndama wa dhahabu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ndipo BWANA akawapiga watu kwa ugonjwa wa tauni kwa sababu ya yale waliyoyafanya kwa ndama yule ambaye alitengenezwa na Aroni.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ndipo bwana akawapiga watu kwa ugonjwa wa tauni kwa sababu ya yale waliyoyafanya kwa ndama yule ambaye alitengenezwa na Haruni.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
BWANA akawapiga hao watu, kwa tauni kwa kuifanya ile ndama, ambayo Haruni aliifanya.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mwenyezi-Mungu akawapelekea watu ugonjwa wa tauni, kwa kuwa walimwomba Aroni awafanyie yule ndama wa dhahabu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ndivyo, Bwana alivyowapiga watu wa huo ukoo kwa kuifanya hiyo ndama, Haroni aliyoifanya.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
BWANA akawapiga hao watu, kwa walivyoifanya ile ndama, ambayo Haruni aliifanya.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Yawe akawaletea watu ugonjwa mukali, kwa kuwa walimwomba Haruni awafanyie yule mwana-ngombe wa zahabu.