Exodus 33:19 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mwenyezi-Mungu akamjibu, “Nitapita mbele yako na kukuonesha wema wangu wote nikilitangaza jina langu, ‘Mwenyezi-Mungu’. Mimi nitamrehemu yule ninayependa kumrehemu, na kumhurumia yule ninayependa kumhurumia.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ndipo Mwenyezi Mungu akasema, “Nitapitisha wema wangu wote mbele yako, nami nitalitangaza Jina langu, Mwenyezi Mungu, mbele ya uso wako. Nitamrehemu yeye nimrehemuye, na pia nitamhurumia yeye nimhurumiaye.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Akasema, Nitapitisha wema wangu wote mbele yako, nami nitalitangaza jina la Bwana mbele yako; nami nitamfadhili yeye nitakayemfadhili; nitamrehemu yeye nitakayemrehemu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mwenyezi-Mungu akamjibu, “Nitapita mbele yako na kukuonesha wema wangu wote nikilitangaza jina langu, ‘Mwenyezi-Mungu’. Mimi nitamrehemu yule ninayependa kumrehemu, na kumhurumia yule ninayependa kumhurumia.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ndipo BWANA akasema, “Nitapitisha wema wangu wote mbele yako, nami nitalitangaza Jina langu, BWANA, mbele ya uso wako. Nitakuwa na rehema kwake yeye nimrehemuye, pia nitakuwa na huruma kwake yeye nimhurumiaye.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ndipo bwana akasema, “Nitapitisha wema wangu wote mbele yako, nami nitalitangaza Jina langu, bwana, mbele ya uso wako. Nitamrehemu yeye nimrehemuye, na pia nitamhurumia yeye nimhurumiaye.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Akasema, Nitapitisha wema wangu wote mbele yako, nami nitalitangaza jina la BWANA mbele yako; nami nitamfadhili yeye nitakayemfadhili; nitamrehemu yeye nitakayemrehemu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mwenyezi-Mungu akamjibu, “Nitapita mbele yako na kukuonesha wema wangu wote nikilitangaza jina langu, ‘Mwenyezi-Mungu’. Mimi nitamrehemu yule ninayependa kumrehemu, na kumhurumia yule ninayependa kumhurumia.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Akaitikia kwamba: Nitaupitisha wema wangu wote machoni pako, nalo Jina langu la Bwana nitalitamka kwa sauti kuu masikioni pako. Mimi nitakayemhurumia, nitamhurumia kweli; nitakayemwonea uchungu, nitamwonea uchungu wa kweli.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Akasema, Nitapitisha wema wangu wote mbele yako, nami nitalitangaza jina la BWANA mbele yako; nami nitamfadhili yeye nitakayemfadhili; nitamrehemu yeye nitakayemrehemu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Yawe akamujibu: Nitapita mbele yako na kukuonyesha uzuri wangu wote nikilitangaza jina langu, Yawe. Mimi nitamuhurumia yule ninayependa kumuhurumia; nitamurehemu yule ninayependa kumurehemu.