Exodus 33:7 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mose alikuwa na desturi ya kulichukua lile hema na kulisimika nje ya kambi. Hema hilo alilipa jina, Hema la Mkutano. Mtu yeyote aliyetaka shauri kwa Mwenyezi-Mungu alikwenda kwenye hema la mkutano nje ya kambi.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Basi Musa alikuwa na desturi ya kuchukua hema na kuliweka wakfu nje ya kambi umbali kiasi, akaliita “Hema la Kukutania”. Kila aliyekuwa akiulizia shauri kwa Mwenyezi Mungu, angeenda hadi Hema la Kukutania, nje ya kambi.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi desturi ya Musa, ilikuwa kuitwaa ile hema, na kuikita nje ya marago mbali na hayo marago; akaiita, hema ya kukutania. Hata kila mtu aliyekuwa akitaka neno kwa Bwana, akatoka, akaenda hata hema ya kukutania, iliyokuwa nje ya marago.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mose alikuwa na desturi ya kulichukua lile hema na kulisimika nje ya kambi. Hema hilo alilipa jina, Hema la Mkutano. Mtu yeyote aliyetaka shauri kwa Mwenyezi-Mungu alikwenda kwenye hema la mkutano nje ya kambi.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Basi Mose alikuwa na desturi ya kuchukua hema na kulisimika nje ya kambi umbali kiasi, akaliita “Hema la Kukutania.” Kila aliyekuwa akiulizia shauri kwa BWANA, angelikwenda katika Hema la Kukutania nje ya kambi.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Basi Musa alikuwa na desturi ya kuchukua hema na kuliweka wakfu nje ya kambi umbali kiasi, akaliita “Hema la Kukutania.” Kila aliyekuwa akiulizia shauri kwa bwana, angelikwenda katika Hema la Kukutania nje ya kambi.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi desturi ya Musa, ilikuwa kuitwaa ile hema, na kuikita nje ya kambi na mbali hiyo kambi; akaiita, hema ya kukutania. Hata kila mtu aliyekuwa akitaka neno kwa BWANA, akatoka, akaenda hata hema ya kukutania, iliyokuwa nje ya kambi.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mose alikuwa na desturi ya kulichukua lile hema na kulisimika nje ya kambi. Hema hilo alilipa jina, Hema la Mkutano. Mtu yeyote aliyetaka shauri kwa Mwenyezi-Mungu alikwenda kwenye hema la mkutano nje ya kambi.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Mose akaambiwa, lile Hema alichukue kila mara, alipige nje ya makambi, iwe mbali ya makambi, nalo aliite Hema la Mkutano, kila atakayemtafuta Bwana atoke kwenda kwenye Hema la Mkutano lililoko nje ya makambi.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi desturi ya Musa, ilikuwa kuitwaa ile hema, na kuikita nje ya marago mbali na hayo marago; akaiita, hema ya kukutania. Hata kila mtu aliyekuwa akitaka neno kwa BWANA, akatoka, akaenda hata hema ya kukutania, iliyokuwa nje ya marago.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Musa alikuwa na desturi ya kuchukua lile hema na kulisimika inje ya kambi. Hema hilo alilipa jina, hema la mukutano. Mutu yeyote aliyetaka shauri kwa Yawe alikwenda kwenye hema la mukutano inje ya kambi.