Exodus 34:20 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mzaliwa wa kwanza wa punda utamkomboa kwa kunitolea kondoo. Kama hutamkomboa utamvunja shingo. Watoto wenu wote wa kiume ambao ni wazaliwa wa kwanza mtawakomboa. Mtu yeyote asije mbele yangu mikono mitupu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Utakomboa mzaliwa wa kwanza wa punda kwa mwana-kondoo, lakini kama humkomboi, utavunja shingo yake. Utakomboa wazaliwa wako wa kwanza wote wa kiume. “Mtu yeyote asije mbele zangu mikono mitupu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na mzaliwa wa kwanza wa punda utamkomboa kwa mwana-kondoo; tena kwamba hutaki kumkomboa, ndipo utamvunja shingo. Wazaliwa wa kwanza wote wa wanao utawakomboa. Wala hapana atakayehudhuria mbele zangu mikono mitupu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mzaliwa wa kwanza wa punda utamkomboa kwa kunitolea kondoo. Kama hutamkomboa utamvunja shingo. Watoto wenu wote wa kiume ambao ni wazaliwa wa kwanza mtawakomboa. Mtu yeyote asije mbele yangu mikono mitupu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Utakomboa mzaliwa wa kwanza wa punda kwa mwana-kondoo, lakini kama humkomboi, utavunja shingo yake. Utakomboa wazaliwa wako wa kwanza wote wa kiume. “Mtu ye yote asije mbele zangu mikono mitupu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Utakomboa mzaliwa wa kwanza wa punda kwa mwana-kondoo, lakini kama humkomboi, utavunja shingo yake. Utakomboa wazaliwa wako wa kwanza wote wa kiume. “Mtu yeyote asije mbele zangu mikono mitupu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na mzaliwa wa kwanza wa punda utamkomboa kwa mwana-kondoo; tena ikiwa hutaki kumkomboa, ndipo utamvunja shingo. Wazaliwa wa kwanza wote wa wanao utawakomboa. Wala hakuna atakayehudhuria mbele zangu mikono mitupu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mzaliwa wa kwanza wa punda utamkomboa kwa kunitolea kondoo. Kama hutamkomboa utamvunja shingo. Watoto wenu wote wa kiume ambao ni wazaliwa wa kwanza mtawakomboa. Mtu yeyote asije mbele yangu mikono mitupu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Mwana wa kwanza wa punda utamkomboa kwa mwana kondoo; usipomkomboa, umvunje shingo! Wana wa kwanza wote watakaozaliwa na wanao sharti uwakomboe. Watu wasinitokee mikono mitupu!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na mzaliwa wa kwanza wa punda utamkomboa kwa mwana-kondoo; tena kwamba hutaki kumkomboa, ndipo utamvunja shingo. Wazaliwa wa kwanza wote wa wanao utawakomboa. Wala hapana atakayehudhuria mbele zangu mikono mitupu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Muzaliwa wa kwanza wa punda utamukomboa kwa kunitolea kondoo. Kama hautamukomboa utamuvunja shingo. Watoto wenu wote wanaume ambao ni wazaliwa wa kwanza mutawakomboa. Mutu yeyote asikuje mbele yangu mikono mitupu.