Exodus 34:24 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Nitayafukuza mataifa mengine mbele yenu na kuipanua mipaka yenu. Hakuna mtu yeyote atakayeitamani nchi yenu wakati mnapokusanyika kuniabudu mimi Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu mara tatu kila mwaka.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Nitawafukuza mataifa mbele yako na kupanua mipaka ya nchi yako, wala hakuna mtu yeyote atakayeitamani nchi yako wakati unapoenda mara tatu kila mwaka kuonana na Mwenyezi Mungu, Mungu wako.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kwa kuwa mimi nitazitupa nje taifa za watu mbele yako, na kuipanua mipaka yako; wala hapana mtu ye yote atakayeitamani nchi yako, hapo utakapokwea kwenda kuhudhuria mbele za Bwana Mungu wako mara tatu kila mwaka.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Nitayafukuza mataifa mengine mbele yenu na kuipanua mipaka yenu. Hakuna mtu yeyote atakayeitamani nchi yenu wakati mnapokusanyika kuniabudu mimi Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu mara tatu kila mwaka.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Nitawafukuza mataifa mbele yako na kupanua mipaka ya nchi yako, wala hakuna mtu ye yote atakayeitamani nchi yako wakati unapokwenda mara tatu kila mwaka kuonana na BWANA Mungu wako.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Nitawafukuza mataifa mbele yako na kupanua mipaka ya nchi yako, wala hakuna mtu yeyote atakayeitamani nchi yako wakati unapokwenda mara tatu kila mwaka kuonana na bwana Mwenyezi Mungu wako.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kwa kuwa mimi nitayatupa nje mataifa ya watu mbele yako, na kuipanua mipaka yako; wala hapana mtu yeyote atakayeitamani nchi yako, hapo utakapokwea kwenda kuhudhuria mbele za BWANA Mungu wako mara tatu kila mwaka.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Nitayafukuza mataifa mengine mbele yenu na kuipanua mipaka yenu. Hakuna mtu yeyote atakayeitamani nchi yenu wakati mnapokusanyika kuniabudu mimi Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu mara tatu kila mwaka.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwani nitawafukuza wamizimu mbele yako, niipanue mipaka yako; hatakuwako mtu atakayeitamani nchi yako, utakapopanda kutokea mbele ya Bwana Mungu wako mara tatu kila mwaka.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kwa kuwa mimi nitazitupa nje taifa za watu mbele yako, na kuipanua mipaka yako; wala hapana mtu ye yote atakayeitamani nchi yako, hapo utakapokwea kwenda kuhudhuria mbele za BWANA Mungu wako mara tatu kila mwaka.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Nitafukuza mataifa mengine mbele yenu na kupanua mipaka yenu. Hakuna mutu yeyote atakayetamani inchi yenu wakati munapokusanyika kwa kuniabudu, mimi Yawe, Mungu wenu, mara tatu kila mwaka.