Exodus 34:28 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mose alikaa huko mlimani pamoja na Mwenyezi-Mungu siku arubaini, mchana na usiku; hakula chakula wala kunywa maji. Aliandika maneno yote ya agano na zile amri kumi.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Musa alikuwa huko pamoja na Mwenyezi Mungu kwa siku arobaini usiku na mchana bila kula chakula wala kunywa maji. Naye akaandika juu ya vibao maneno ya agano, yaani zile Amri Kumi.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Naye alikuwa huko pamoja na Bwana siku arobaini na masiku yake; hakula chakula, wala hakunywa maji. Naye akaandika katika hizo mbao, hayo maneno ya maagano, hizo amri kumi.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mose alikaa huko mlimani pamoja na Mwenyezi-Mungu siku arubaini, mchana na usiku; hakula chakula wala kunywa maji. Aliandika maneno yote ya agano na zile amri kumi.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Mose alikuwa huko pamoja na BWANA kwa siku arobaini mchana na usiku bila kula chakula wala kunywa maji. Naye akaandika juu ya vibao maneno ya Agano, yaani zile Amri Kumi.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Musa alikuwa huko pamoja na bwana kwa siku arobaini usiku na mchana bila kula chakula wala kunywa maji. Naye akaandika juu ya vibao maneno ya Agano, yaani zile Amri Kumi.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Naye alikuwa huko pamoja na BWANA siku arobaini na masiku yake; hakula chakula, wala hakunywa maji. Naye akaandika katika hizo mbao, hayo maneno ya maagano, hizo amri kumi.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mose alikaa huko mlimani pamoja na Mwenyezi-Mungu siku arubaini, mchana na usiku; hakula chakula wala kunywa maji. Aliandika maneno yote ya agano na zile amri kumi.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Akawa huko pamoja na Bwana siku 40 mchana na usiku, hakula chakula, wala hakunywa maji, akaandika katika zile mbao mbili maneno ya Agano hili, ndiyo yale maagizo kumi.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Naye alikuwa huko pamoja na BWANA siku arobaini na masiku yake; hakula chakula, wala hakunywa maji. Naye akaandika katika hizo mbao, hayo maneno ya maagano, hizo amri kumi.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Musa alikaa kule kwenye mulima pamoja na Yawe siku makumi ine, muchana na usiku. Hakukula chakula wala kunywa maji. Aliandika maneno yote ya agano na zile amri kumi.