Exodus 34:3 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mtu yeyote asije pamoja nawe, wala asionekane popote mlimani; wala kondoo au ng'ombe wasilishwe karibu yake.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mtu yeyote asije nawe, wala asionekane mtu popote mlimani; wala kondoo na mbuzi au ng’ombe wasilishe mbele ya huo mlima.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Asikwee mtu pamoja nawe, wala asionekane mtu awaye yote katika huo mlima; wala kondoo na ng'ombe wasilishe mbele ya huo mlima.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mtu yeyote asije pamoja nawe, wala asionekane popote mlimani; wala kondoo au ng'ombe wasilishwe karibu yake.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Mtu ye yote asije pamoja nawe, wala asionekane mtu po pote juu ya mlima, wala kondoo na mbuzi au ng'ombe wasilishe karibu mbele ya huo mlima.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Mtu yeyote asije pamoja nawe, wala asionekane mtu popote juu ya mlima, wala kondoo na mbuzi au ng’ombe wasilishe karibu mbele ya huo mlima.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Asikwee mtu pamoja nawe, wala asionekane mtu yeyote katika huo mlima; wala kondoo na ng'ombe wasilishwe mbele ya huo mlima.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mtu yeyote asije pamoja nawe, wala asionekane popote mlimani; wala kondoo au ng'ombe wasilishwe karibu yake.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Asipande mtu pamoja na wewe, wala asionekane mtu mlimani po pote, wala kondoo wala mbuzi wala ng'ombe wasilishe penye mlima huu!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Asikwee mtu pamoja nawe, wala asionekane mtu awaye yote katika huo mlima; wala kondoo na ng’ombe wasilishe mbele ya huo mlima.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mutu yeyote asikuje pamoja nawe, wala asionekane popote kwenye mulima, wala kondoo au ngombe wasikulishwe karibu yake.