Exodus 34:9 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kisha akasema, “Ee Bwana wangu, kwa vile umenijalia fadhili mbele zako, nakuomba uende pamoja nasi. Watu hawa ni wenye vichwa vigumu, lakini utusamehe uovu wetu na dhambi yetu, utupokee kama watu wako mwenyewe.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Musa akasema, “Ee Bwana, kama nimepata kibali mbele zako, basi Bwana uende pamoja nasi. Ingawa watu hawa ni wenye shingo ngumu, samehe uovu wetu na dhambi yetu, tuchukue kuwa urithi wako.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Akasema, Ikiwa sasa nimepata neema mbele zako, Bwana, nakuomba, Bwana, uende kati yetu, maana ni watu wenye shingo ngumu; ukasamehe uovu wetu na dhambi yetu, ukatutwae tuwe urithi wako.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kisha akasema, “Ee Bwana wangu, kwa vile umenijalia fadhili mbele zako, nakuomba uende pamoja nasi. Watu hawa ni wenye vichwa vigumu, lakini utusamehe uovu wetu na dhambi yetu, utupokee kama watu wako mwenyewe.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Mose akasema, “Ee BWANA, kama nimepata kibali mbele zako, basi BWANA uende pamoja nasi. Ingawa watu hawa ni wenye shingo ngumu, samehe uovu wetu na dhambi yetu, tuchukue kuwa urithi wako.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Musa akasema, “Ee bwana, kama nimepata kibali mbele zako, basi bwana uende pamoja nasi. Ingawa watu hawa ni wenye shingo ngumu, samehe uovu wetu na dhambi yetu, tuchukue kuwa urithi wako.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Akasema, Ikiwa sasa nimepata neema mbele zako, Bwana, nakuomba, Bwana, uende kati yetu, maana ni watu wenye shingo ngumu; ukasamehe uovu wetu na dhambi yetu, ukatutwae tuwe urithi wako.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kisha akasema, “Ee Bwana wangu, kwa vile umenijalia fadhili mbele zako, nakuomba uende pamoja nasi. Watu hawa ni wenye vichwa vigumu, lakini utusamehe uovu wetu na dhambi yetu, utupokee kama watu wako mwenyewe.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
akasema: Bwana wangu, kama nimeona upendeleo machoni pako, Bwana wangu na aende katikati yetu! Kwani watu hawa ni wenye kosi ngumu. Nawe tuondolee manza zetu na makosa yetu na kutupokea kuwa wako!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Akasema, Ikiwa sasa nimepata neema mbele zako, Bwana, nakuomba, Bwana, uende kati yetu, maana ni watu wenye shingo ngumu; ukasamehe uovu wetu na dhambi yetu, ukatutwae tuwe urithi wako.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kisha akasema: Ee Bwana wangu, kama nimepata kukubaliwa mbele yako, ninakuomba uende pamoja nasi. Watu hawa ni wenye vichwa vigumu, lakini utusamehe uovu wetu na zambi yetu, utupokee kama watu wako mwenyewe.