Exodus 35:22 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Hivyo wote wenye moyo mkarimu, wanaume kwa wanawake, wakaleta vipini, pete za mhuri, vikuku na kila aina ya vyombo vya dhahabu; kila mtu akamtolea Mwenyezi-Mungu kitu cha dhahabu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Wote waliopenda, wanaume na wanawake, wakaja wakaleta vito vya dhahabu vya kila aina: vipini, vipuli, pete na mapambo. Wote wakatoa dhahabu zao kuwa sadaka ya kuinuliwa kwa Mwenyezi Mungu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Nao wakaja, waume kwa wake, wote waliokuwa na moyo wa kupenda, wakaleta vipini, na hazama, na pete za muhuri, na vikuku, na vyombo vyote vya dhahabu; kila mtu aliyetoa toleo la dhahabu la kumpa Bwana.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Hivyo wote wenye moyo mkarimu, wanaume kwa wanawake, wakaleta vipini, pete za mhuri, vikuku na kila aina ya vyombo vya dhahabu; kila mtu akamtolea Mwenyezi-Mungu kitu cha dhahabu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Wote waliokuwa na utayari, wanaume kwa wanawake, wakaja wakaleta vito vya dhahabu vya kila aina: vipini, vipuli, pete na mapambo. Wote wakatoa dhahabu zao kama sadaka ya kuinuliwa kwa BWANA.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Wote waliokuwa na utayari, wanaume kwa wanawake, wakaja wakaleta vito vya dhahabu vya kila aina: vipini, vipuli, pete na mapambo. Wote wakatoa dhahabu zao kama sadaka ya kuinuliwa kwa bwana.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Nao wakaja, wanaume kwa wanawake, wote waliokuwa na moyo wa kupenda, wakaleta vipini, hazama, pete za mhuri, vikuku na vyombo vyote vya dhahabu; kila mtu aliyetoa toleo la dhahabu la kumpa BWANA.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Hivyo wote wenye moyo mkarimu, wanaume kwa wanawake, wakaleta vipini, pete za mhuri, vikuku na kila aina ya vyombo vya dhahabu; kila mtu akamtolea Mwenyezi-Mungu kitu cha dhahabu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Wakaja waume kwa wake, maana wote walitumwa na mioyo yao, wakaleta vipini na mapete ya masikioni na pete za vidoleni na mapambo yo yote ya dhahabu; tena kila mtu akaleta dhahabu kuwa vipaji vya tambiko vya kupitishwa motoni vya kumpa Bwana.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Nao wakaja, waume kwa wake, wote waliokuwa na moyo wa kupenda, wakaleta vipini, na hazama, na pete za muhuri, na vikuku, na vyombo vyote vya dhahabu; kila mtu aliyetoa toleo la dhahabu la kumpa BWANA.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Hivyo wote wenye moyo safi, wanaume na wanawake, wakaleta pete za masikio na za muhuri, vikuku na kila aina ya mapambo ya zahabu. Kila mutu akamutolea Yawe kitu cha zahabu.