Exodus 35:29 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Waisraeli wote, wanaume kwa wanawake, ambao walivutwa moyoni mwao kuleta chochote kwa ajili ya kazi ambayo Mwenyezi-Mungu alikuwa amemwagiza Mose ifanyike, walileta vitu hivyo kwa hiari, kama mchango wa kumpa Mwenyezi-Mungu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Waisraeli wote, wanaume na wanawake, waliopenda wakaleta mbele za Mwenyezi Mungu kwa hiari yao wenyewe sadaka kwa ajili ya kazi yote ya Mwenyezi Mungu aliyokuwa amewaagiza kuifanya kupitia kwa Musa.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Wana wa Israeli wakaleta sadaka za kumpa Bwana kwa moyo wa kupenda; wote, waume kwa wake, ambao mioyo yao iliwafanya kuwa wapenda kuleta kwa hiyo kazi, ambayo Bwana aliamuru ifanywe kwa mkono wa Musa.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Waisraeli wote, wanaume kwa wanawake, ambao walivutwa moyoni mwao kuleta chochote kwa ajili ya kazi ambayo Mwenyezi-Mungu alikuwa amemwagiza Mose ifanyike, walileta vitu hivyo kwa hiari, kama mchango wa kumpa Mwenyezi-Mungu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Waisraeli wote waume kwa wake waliokuwa wanapenda wakaleta mbele za BWANA kwa hiari yao wenyewe sadaka kwa ajili ya kazi yote ya BWANA aliyokuwa amewaagiza kuifanya kupitia kwa Mose.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Waisraeli wote waume kwa wake waliokuwa wanapenda wakaleta mbele za bwana kwa hiari yao wenyewe sadaka kwa ajili ya kazi yote ya bwana aliyokuwa amewaagiza kuifanya kupitia kwa Musa.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Wana wa Israeli wakaleta sadaka za kumpa BWANA kwa moyo wa kupenda; wote, wanaume kwa wanawake, ambao mioyo yao iliwafanya kuwa wapenda kuleta kwa hiyo kazi, ambayo BWANA aliamuru ifanywe kwa mkono wa Musa.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Waisraeli wote, wanaume kwa wanawake, ambao walivutwa moyoni mwao kuleta chochote kwa ajili ya kazi ambayo Mwenyezi-Mungu alikuwa amemwagiza Mose ifanyike, walileta vitu hivyo kwa hiari, kama mchango wa kumpa Mwenyezi-Mungu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Hivyo wakachanga wana wa Isiraeli wote, waume kwa wake, waliotumwa na mioyo yao kuyapeleka yafaayo ya kufanya kazi zote, Bwana alizoziagiza kinywani mwa Mose, zifanywe.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Wana wa Israeli wakaleta sadaka za kumpa BWANA kwa moyo wa kupenda; wote, waume kwa wake, ambao mioyo yao iliwafanya kuwa wapenda kuleta kwa hiyo kazi, ambayo BWANA aliamuru ifanywe kwa mkono wa Musa.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Waisraeli wote, wanaume na wanawake, ambao walivutwa ndani ya moyo wao kuleta kitu chochote kwa ajili ya kazi ambayo Yawe alikuwa amemwagiza Musa ifanyike, walileta vitu hivyo kwa mapenzi yao, kama vile muchango wa kumupa Yawe.