Exodus 36:11 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Alitengeneza vitanzi vya buluu upindoni mwa pazia la mwisho la kipande cha kwanza, na vitanzi vingine katika pazia la mwisho la kipande cha pili.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kisha wakatengeneza vitanzi vya kitambaa cha buluu kwenye upindo wa pazia la mwisho la fungu la kwanza, pia wakafanya vivyo hivyo na pazia la fungu la mwisho.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kisha akafanya matanzi ya rangi ya samawi katika ncha za pazia moja, katika upindo wa kiungo chake; akafanya vivyo katika ncha ya pazia lililokuwa upande wa nje katika kiungo cha pili.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Alitengeneza vitanzi vya buluu upindoni mwa pazia la mwisho la kipande cha kwanza, na vitanzi vingine katika pazia la mwisho la kipande cha pili.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kisha wakatengeneza vitanzi vya buluu kwenye upindo wa pazia la mwisho la kipande cha kwanza, na vitanzi vingine katika pazia la mwisho la kipande cha pili.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kisha wakatengeneza vitanzi vya kitambaa cha buluu kwenye upindo wa pazia la mwisho la fungu la kwanza, pia wakafanya vivyo hivyo na pazia la fungu la mwisho.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kisha akafanya matanzi ya rangi ya buluu katika ncha za pazia moja, katika upindo wa kiungo chake; akafanya vivyo hivyo katika ncha ya pazia lililokuwa upande wa nje katika kiungo cha pili.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Alitengeneza vitanzi vya buluu upindoni mwa pazia la mwisho la kipande cha kwanza, na vitanzi vingine katika pazia la mwisho la kipande cha pili.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kisha akashona vitanzi vya nguo nyeusi za kifalme penye upindo wa nje wa kila pazia moja hapo, lilipoungwa na jingine; vivyo hivyo akavitia napo penye yupindo wa nje wa kila pazia la pili hapo, lilipoungwa nalo la kwanza.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kisha akafanya matanzi ya rangi ya samawi katika ncha za pazia moja, katika upindo wa kiungo chake; akafanya vivyo katika ncha ya pazia lililokuwa upande wa nje katika kiungo cha pili.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Alitengeneza kamba za rangi ya samawi kwenye upindo wa pazia la mwisho la kipande cha kwanza na kamba zingine katika pazia la mwisho la kipande cha pili.