Exodus 36:29 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mbao hizo mbili za pembeni ziliachana chini lakini zilishikamanishwa kwenye pete ya kwanza. Mbao mbili kwa ajili ya hizo pembe mbili zilitengenezwa namna hiyo.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Katika pembe hizi mbili mihimili yake ilikuwa miwili kuanzia chini hadi juu, na ikaingizwa kwenye pete moja; mihimili ya pembe hizi mbili ilifanana.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Nazo zilikuwa mbao pacha upande wa chini, vivyo zilishikamana pamoja hata ncha ya juu kufikilia pete ya kwanza; ndivyo alivyofanya zote mbili katika hizo pembe mbili.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mbao hizo mbili za pembeni ziliachana chini lakini zilishikamanishwa kwenye pete ya kwanza. Mbao mbili kwa ajili ya hizo pembe mbili zilitengenezwa namna hiyo.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Katika pembe hizi mbili mihimili yake ilikuwa jozi moja kuanzia chini mpaka juu, na ikaingizwa kwenye pete moja; jozi zote mbili zilikuwa za kufanana.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Katika pembe hizi mbili mihimili yake ilikuwa miwili kuanzia chini mpaka juu, na ikaingizwa kwenye pete moja; mihimili ya pembe hizi mbili ilifanana.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Nazo zilikuwa mbao pacha upande wa chini, vivyo hivyo zilishikamana pamoja hata ncha ya juu kufikia pete ya kwanza; ndivyo alivyofanya zote mbili katika hizo pembe mbili.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mbao hizo mbili za pembeni ziliachana chini lakini zilishikamanishwa kwenye pete ya kwanza. Mbao mbili kwa ajili ya hizo pembe mbili zilitengenezwa namna hiyo.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nazo zilikuwa kama pacha, toka chini viliendelea pamoja zote nzima mpaka juu penye pete la kwanza; hivyo ndivyo, alivyozitengeneza mbao zote mbili za hizo pembe mbili za nyuma.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Nazo zilikuwa mbao pacha upande wa chini, vivyo zilishikamana pamoja hata ncha ya juu kufikilia pete ya kwanza; ndivyo alivyofanya zote mbili katika hizo pembe mbili.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mbao hizo mbili za pembeni ziliachana chini lakini zilishikamanishwa kwenye pete ya kwanza. Mbao mbili kwa ajili ya hizo pembe mbili zilitengenezwa namna hiyo.