Exodus 37:17 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Alitengeneza pia kinara cha taa kwa dhahabu safi. Tako lake, na ufito wa hicho kinara ulikuwa kitu kimoja pamoja na vikombe vyake, matumba yake na maua yake.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Akatengeneza kinara cha taa cha dhahabu safi iliyofuliwa vizuri katika kitako chake na ufito wake; vikombe vyake vilivyofanana na ua, matovu na maua vilikuwa kitu kimoja.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kisha akakifanya kile kinara cha taa cha dhahabu safi, akakifanya kile kinara cha taa cha kazi ya kufua, tako lake, na mti wake; vikombe vyake, na matovu yake, na maua yake, vyote vilikuwa vya kitu kimoja nacho,
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Alitengeneza pia kinara cha taa kwa dhahabu safi. Tako lake, na ufito wa hicho kinara ulikuwa kitu kimoja pamoja na vikombe vyake, matumba yake na maua yake.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Akatengeneza kinara cha taa kwa dhahabu safi iliyofuliwa vizuri, kitako chake na ufito, vikombe vyake vilivyofanana na ua, matovu na maua vilikuwa vya kitu kimoja.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Akatengeneza kinara cha taa cha dhahabu safi iliyofuliwa vizuri katika kitako chake na ufito wake; vikombe vyake vilivyofanana na ua, matovu na maua vilikuwa kitu kimoja.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kisha akakifanya kile kinara cha taa cha dhahabu safi, akakifanya kile kinara cha taa cha kazi ya kufua, kitako chake, na mti wake; vikombe vyake, matovu yake, na maua yake, vyote vilikuwa vya kitu kimoja nacho,
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Alitengeneza pia kinara cha taa kwa dhahabu safi. Tako lake, na ufito wa hicho kinara ulikuwa kitu kimoja pamoja na vikombe vyake, matumba yake na maua yake.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kisha akatengeneza kinara cha dhahabu tupu; hicho kinara nacho akakitengeneza kwa kufuafua dhahabu, ikapata kukitoka chote kizima: shina lake na mti wake navyo vikombe vyake na vifundo vyake na maua yake, vyote pia vilikuwa vimetoka dhahabu iyo hiyo moja.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kisha akakifanya kile kinara cha taa cha dhahabu safi, akakifanya kile kinara cha taa cha kazi ya kufua, tako lake, na mti wake; vikombe vyake, na matovu yake, na maua yake, vyote vilikuwa vya kitu kimoja nacho,
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Akatengeneza vilevile kinara cha taa kwa zahabu safi. Tako lake na muti wa hicho kinara ulikuwa kitu kimoja pamoja na vikombe vyake, vifundo vyake na maua yake.