Exodus 37:21 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mahali pale palipotokezea jozi tatu za matawi chini ya kila jozi kulikuwa na tumba moja.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Tovu moja lilikuwa chini ya jozi ya kwanza ya matawi yaliyotokeza kwenye kinara cha taa, tovu la pili chini ya jozi ya pili, nalo tovu la tatu chini ya jozi ya tatu, yaani matawi sita kwa jumla.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
kisha chini ya matawi mawili mlikuwa na tovu iliyokuwa ya kitu kimoja nacho, na chini ya matawi mawili mengine mlikuwa na tovu ya kitu kimoja nacho, tena chini ya matawi mawili hayo mengine mlikuwa na tovu ya kitu kimoja nacho; kwa ajili ya hayo matawi sita, yaliyotokana nacho.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mahali pale palipotokezea jozi tatu za matawi chini ya kila jozi kulikuwa na tumba moja.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Tovu moja lilikuwa chini ya jozi ya kwanza ya matawi yaliyojitokeza kwenye kinara cha taa, tovu la pili chini ya jozi ya pili, nalo tovu la tatu chini ya jozi ya tatu, yaani, jumla matawi sita.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Tovu moja lilikuwa chini ya jozi ya kwanza ya matawi yaliyotokeza kwenye kinara cha taa, tovu la pili chini ya jozi ya pili, nalo tovu la tatu chini ya jozi ya tatu, yaani, matawi sita kwa jumla.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
kisha chini ya matawi mawili mlikuwa na tovu iliyokuwa ya kitu kimoja nacho, na chini ya matawi mawili mengine mlikuwa na tovu ya kitu kimoja nacho, tena chini ya matawi mawili hayo mengine mlikuwa na tovu ya kitu kimoja nacho; kwa ajili ya hayo matawi sita, yaliyotokana nacho.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mahali pale palipotokezea jozi tatu za matawi chini ya kila jozi kulikuwa na tumba moja.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Tena kila mahali matawi mawili yalipotoka katika huo mti wake, chini yake kilikuwa kifundo kimoja; vilikuwa vivyo hivyo kila mahali, yalipotoka matawi mawili, nayo matawi yaliyotoka katika kinara yalikuwa sita.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
kisha chini ya matawi mawili mlikuwa na tovu iliyokuwa ya kitu kimoja nacho, na chini ya matawi mawili mengine mlikuwa na tovu ya kitu kimoja nacho, tena chini ya matawi mawili hayo mengine mlikuwa na tovu ya kitu kimoja nacho; kwa ajili ya hayo matawi sita, yaliyotokana nacho.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kulikuwa kifundo kila pahali matawi mawilimawili yalipotokea kufuatana na yale matawi sita yanayotoka kwa kile kinara.