Exodus 37:25 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Alitengeneza madhabahu ya kufukizia ubani kwa mbao za mjohoro. Madhabahu hiyo ilikuwa ya mraba, sentimita 45 kwa sentimita 45, na kimo chake sentimita 90. Pembe za madhabahu hiyo zilikuwa kitu kimoja na madhabahu yenyewe.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Akatengeneza madhabahu ya kufukizia uvumba kwa mbao za mshita. Ilikuwa ya mraba, urefu na upana wake dhiraa moja, na kimo cha dhiraa mbili, nazo pembe zake zilikuwa kitu kimoja nayo.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kisha akafanya hiyo madhabahu ya kufukizia uvumba ya mti wa mshita; urefu wake ulikuwa ni dhiraa moja, na upana wake ulikuwa ni dhiraa moja, ilikuwa mraba; na kwenda juu kwake kulikuwa ni dhiraa mbili; na pembe zake zilikuwa za kitu kimoja nayo.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Alitengeneza madhabahu ya kufukizia ubani kwa mbao za mjohoro. Madhabahu hiyo ilikuwa ya mraba, sentimita 45 kwa sentimita 45, na kimo chake sentimita 90. Pembe za madhabahu hiyo zilikuwa kitu kimoja na madhabahu yenyewe.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Akatengeneza madhabahu ya kufukiza uvumba kwa mbao za mshita. Ilikuwa ya mraba, urefu wake dhiraa moja, upana wake dhiraa moja, na kimo chake dhiraa mbili: pembe zake zilikuwa za kitu kimoja nayo.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Akatengeneza madhabahu ya kufukizia uvumba kwa mbao za mshita. Ilikuwa ya mraba, urefu na upana wake dhiraa moja, na kimo cha dhiraa mbili, nazo pembe zake zilikuwa kitu kimoja nayo.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kisha akafanya hiyo madhabahu ya kufukizia uvumba ya mti wa mshita; urefu wake ulikuwa ni dhiraa moja, na upana wake ulikuwa ni dhiraa moja, ilikuwa mraba; na kwenda juu kwake kulikuwa ni dhiraa mbili; na pembe zake zilikuwa za kitu kimoja nayo.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Alitengeneza madhabahu ya kufukizia ubani kwa mbao za mjohoro. Madhabahu hiyo ilikuwa ya mraba, sentimita 45 kwa sentimita 45, na kimo chake sentimita 90. Pembe za madhabahu hiyo zilikuwa kitu kimoja na madhabahu yenyewe.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kisha akatengeneza kwa migunga meza ya kuvukizia; urefu wake ulikuwa mkono mmoja, nao upana wake ulikuwa mkono mmoja, pande zote nne zilikuwa sawa, nao urefu wake wa kwenda juu ulikuwa mikono miwili.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kisha akafanya hiyo madhabahu ya kufukizia uvumba ya mti wa mshita; urefu wake ulikuwa ni dhiraa moja, na upana wake ulikuwa ni dhiraa moja, ilikuwa mraba; na kwenda juu kwake kulikuwa ni dhiraa mbili; na pembe zake zilikuwa za kitu kimoja nayo.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Akatengeneza mazabahu ya kufukizia ubani kwa mbao za mujohoro. Mazabahu hiyo ilikuwa ya muraba, sentimetre makumi ine na tano kwa sentimetre makumi ine na tano, na urefu kwenda juu sentimetre makumi tisa. Pembe za mazabahu hiyo zilikuwa kitu kimoja na mazabahu yenyewe.