Exodus 37:7 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Alitengeneza pia viumbe wenye mabawa wawili kwa kufua dhahabu kwenye miisho ya kifuniko hicho;
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kisha akatengeneza makerubi wawili wa dhahabu iliyofuliwa katika miisho ya hicho kifuniko.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kisha akafanya makerubi mawili ya dhahabu; akayafanya ya kazi ya kufua, yawe katika miisho miwili ya kiti cha rehema;
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Alitengeneza pia viumbe wenye mabawa wawili kwa kufua dhahabu kwenye miisho ya kifuniko hicho;
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kisha akatengeneza makerubi mawili kwenye miisho ya kile kifuniko kutokana na dhahabu iliyofuliwa.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kisha akatengeneza makerubi wawili wa dhahabu iliyofuliwa katika miisho ya hicho kifuniko.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kisha akafanya makerubi mawili ya dhahabu; akayafanya ya kazi ya kufua, yawe katika miisho miwili ya kiti cha rehema;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Alitengeneza pia viumbe wenye mabawa wawili kwa kufua dhahabu kwenye miisho ya kifuniko hicho;
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kisha akatengeneza Makerubi mawili ya dhahabu, nayo yalitengenezwa kwa kuzifuafua hizo dhahabu, akayaweka pande zote mbili za mwisho wa Kiti cha Upozi:
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kisha akafanya makerubi mawili ya dhahabu; akayafanya ya kazi ya kufua, yawe katika miisho miwili ya kiti cha rehema;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Akatengeneza vilevile makerubi wawili kwa kufua zahabu kwenye miisho ya kifuniko hicho;