Exodus 38:12 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Upande wa magharibi ulikuwa na chandarua chenye urefu wa mita 22, nguzo zake 10 na vikalio vyake 10. Kulabu za nguzo na vitanzi vyake vilikuwa vya fedha.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Upande wa mwisho wa magharibi ulikuwa na upana wa dhiraa hamsini, na ulikuwa na mapazia, na nguzo kumi na vitako vyake kumi, pamoja na kulabu na tepe za fedha juu ya hizo nguzo.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Upande wa magharibi mlikuwa na chandarua ya dhiraa hamsini, nguzo zake zilikuwa ni kumi, na matako yake kumi; kulabu za hizo nguzo na vitanzi vyake vilikuwa vya fedha.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Upande wa magharibi ulikuwa na chandarua chenye urefu wa mita 22, nguzo zake 10 na vikalio vyake 10. Kulabu za nguzo na vitanzi vyake vilikuwa vya fedha.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Upande wa mwisho wa magharibi ulikuwa na upana wa dhiraa hamsini na ulikuwa na mapazia, pamoja na nguzo kumi na vitako kumi, pamoja na kulabu za fedha na tepe za fedha juu yake.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Upande wa mwisho wa magharibi ulikuwa na upana wa dhiraa hamsini na ulikuwa na mapazia, na nguzo kumi na vitako vyake kumi, pamoja na kulabu na tepe za fedha juu ya hizo nguzo.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Upande wa magharibi mlikuwa na chandarua ya dhiraa hamsini, nguzo zake zilikuwa ni kumi, na vitako vyake kumi; kulabu za hizo nguzo na vitanzi vyake vilikuwa vya fedha.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Upande wa magharibi ulikuwa na chandarua chenye urefu wa mita 22, nguzo zake 10 na vikalio vyake 10. Kulabu za nguzo na vitanzi vyake vilikuwa vya fedha.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nao upande wa ua unaoelekea baharini ulikuwa wenye nguo za mikono hamsini, nazo nguzo zake zilikuwa kumi zenye miguu kumi, navyo vifungo vya nguzo na vijiti vyao vya kuziungia juu vilikuwa vya fedha.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Upande wa magharibi mlikuwa na chandarua ya dhiraa hamsini, nguzo zake zilikuwa ni kumi, na matako yake kumi; kulabu za hizo nguzo na vitanzi vyake vilikuwa vya fedha.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Upande wa magaribi ulikuwa na pazia yenye urefu wa metre makumi mbili na mbili, nguzo zake kumi na vikalio vyake kumi. Vifungio vya nguzo na kamba zake vilikuwa vya feza.