Exodus 38:17 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Vikalio vyote vya nguzo vilikuwa vya shaba, lakini kulabu za nguzo hizo na vitanzi vyake vilikuwa vya fedha. Matumba yake yalikuwa ya fedha; pia nguzo zake zote zilishikamanishwa kwa fito za fedha.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Vitako vya nguzo vilikuwa vya shaba. Kulabu na tepe juu ya nguzo zilikuwa za fedha, na ncha zake zilifunikwa kwa fedha. Kwa hiyo nguzo zote za ua zilikuwa na tepe za fedha.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na matako ya zile nguzo yalikuwa ya shaba; kulabu za hizo nguzo na vitanzi vyake vilikuwa vya fedha; na vichwa vya zile nguzo vilikuwa ni vya fedha; na nguzo zote za huo ua ziliungwa kwa vitanzi vya fedha.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Vikalio vyote vya nguzo vilikuwa vya shaba, lakini kulabu za nguzo hizo na vitanzi vyake vilikuwa vya fedha. Matumba yake yalikuwa ya fedha; pia nguzo zake zote zilishikamanishwa kwa fito za fedha.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Vitako vya nguzo vilikuwa vya shaba. Kulabu na tepe juu ya nguzo zilikuwa za fedha, ncha zake zilifunikwa kwa fedha, kwa hiyo nguzo yote ya ua ilikuwa na tepe za fedha.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Vitako vya nguzo vilikuwa vya shaba. Kulabu na tepe juu ya nguzo zilikuwa za fedha, na ncha zake zilifunikwa kwa fedha. Kwa hiyo nguzo zote za ua zilikuwa na tepe za fedha.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na vitako vya zile nguzo vilikuwa vya shaba; kulabu za hizo nguzo na vitanzi vyake vilikuwa vya fedha; na vichwa vya zile nguzo vilikuwa ni vya fedha; na nguzo zote za huo ua ziliungwa kwa vitanzi vya fedha.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Vikalio vyote vya nguzo vilikuwa vya shaba, lakini kulabu za nguzo hizo na vitanzi vyake vilikuwa vya fedha. Matumba yake yalikuwa ya fedha; pia nguzo zake zote zilishikamanishwa kwa fito za fedha.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Miguu ya nguzo ilikuwa ya shaba, lakini vifungo vya nguzo na vijiti vyao vya kuziungia juu vilikuwa vya fedha, navyo vichwa vyao walivifunikiza fedha, nazo nguzo zote za ua zilikuwa zimeungwa kwa vijiti vya fedha.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na matako ya zile nguzo yalikuwa ya shaba; kulabu za hizo nguzo na vitanzi vyake vilikuwa vya fedha; na vichwa vya zile nguzo vilikuwa ni vya fedha; na nguzo zote za huo ua ziliungwa kwa vitanzi vya fedha.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Vikalio vyote vya nguzo vilikuwa vya shaba, lakini vifungio vya nguzo hizo na kamba zake vilikuwa vya feza. Vifungio vyake vilikuwa vya feza; vilevile nguzo zake zote zilishikamanishwa kwa fito za feza.