Exodus 38:18 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Pazia la mlango wa ua lilitengenezwa kwa sufu ya rangi ya buluu, zambarau na nyekundu, na kitani safi iliyosokotwa, na kutariziwa vizuri; nalo lilikuwa na urefu wa mita 9 na kimo cha mita 2, kulingana na vyandarua vya ua.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Pazia la ingilio la ua lilikuwa la nyuzi za rangi ya buluu, za zambarau, na za rangi nyekundu pamoja na kitani iliyosokotwa vizuri, kazi ya mtarizi. Pazia hilo lilikuwa na urefu wa dhiraa ishirini kama zile za kwenye ua, na kimo chake kilikuwa dhiraa tano,
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na hilo pazia la lango la ua, lilikuwa ni kazi ya mwenye kutia taraza, lilikuwa la nyuzi za rangi ya samawi, na za rangi ya zambarau, na nyekundu, na kitani nzuri ya kusokotwa; lilikuwa na urefu wake dhiraa ishirini, na kutukuka kwake katika huo upana wake kulikuwa dhiraa tano, kupatana na ile chandarua ya ua.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Pazia la mlango wa ua lilitengenezwa kwa sufu ya rangi ya buluu, zambarau na nyekundu, na kitani safi iliyosokotwa, na kutariziwa vizuri; nalo lilikuwa na urefu wa mita 9 na kimo cha mita 2, kulingana na vyandarua vya ua.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Pazia la kwenye ingilio la ua lilikuwa la kitani lililosokotwa vizuri la rangi ya buluu, ya zambarau, na nyekundu, kazi ya mtarizi. Pazia hilo lilikuwa na urefu wa dhiraa ishirini kama yale ya kwenye ua, kwenda juu kwake lilikuwa dhiraa tano,
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Pazia la ingilio la ua lilikuwa la nyuzi za rangi ya buluu, za zambarau, na za rangi nyekundu pamoja na kitani iliyosokotwa vizuri, kazi ya mtarizi. Pazia hilo lilikuwa na urefu wa dhiraa ishirini kama zile za kwenye ua, na kimo chake kilikuwa dhiraa tano,
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na hilo pazia la lango la ua, lilikuwa ni kazi ya mwenye kutia taraza, lilikuwa la nyuzi za rangi ya buluu, zambarau na nyekundu, na kitani nzuri ya kusokotwa; lilikuwa na urefu wa dhiraa ishirini, na kutukuka kwake katika huo upana wake kulikuwa dhiraa tano, kupatana na ile chandarua ya ua.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Pazia la mlango wa ua lilitengenezwa kwa sufu ya rangi ya buluu, zambarau na nyekundu, na kitani safi iliyosokotwa, na kutariziwa vizuri; nalo lilikuwa na urefu wa mita 9 na kimo cha mita 2, kulingana na vyandarua vya ua.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Hapo penye lango la ua palikuwa na pazia lililokuwa kazi ya fundi wa kufuma kwa nyuzi za rangi, nalo lilitengenezwa kwa nguo za kifalme nyeusi na nyekundu na kwa nguo za bafta ngumu, urefu ulikuwa mikono ishirini, nao upana wa kwenda juu ulikuwa mikono mitano, sawasawa kama nguo nyingine za ua.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na hilo pazia la lango la ua, lilikuwa ni kazi ya mwenye kutia taraza, lilikuwa la nyuzi za rangi ya samawi, na za rangi ya zambarau, na nyekundu, na kitani nzuri ya kusokotwa; lilikuwa na urefu wake dhiraa ishirini, na kutukuka kwake katika huo upana wake kulikuwa dhiraa tano, kupatana na ile chandarua ya ua.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Pazia la mulango wa upango lilitengenezwa kwa sufu ya rangi ya samawi, zambarau na nyekundu, na kitani safi iliyosokotwa, na kupambwa vizuri. Nalo lilikuwa na urefu wa metre tisa na urefu kwenda juu metre mbili, kulingana na mapazia ya upango.