Exodus 38:21 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Ifuatayo ni orodha ya vifaa vilivyotumika katika kulijenga hema takatifu, yaani hema la agano. Orodha hii ilitayarishwa na Walawi kwa amri ya Mose, chini ya uongozi wa Ithamari, mwana wa kuhani Aroni.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ifuatayo ni orodha ya vifaa vilivyotumika kwa ajili ya ujenzi wa maskani ya Mungu, hiyo Maskani ya Ushuhuda, ambavyo vilitayarishwa na Walawi kama alivyoagiza Musa, chini ya usimamizi wa Ithamari, mwana wa kuhani Haruni.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Jumla ya vile vyombo vilivyofanywa kwa ajili ya hiyo maskani, hiyo maskani ya ushuhuda ni hii, kama vilivyohesabiwa, kama maagizo ya Musa yalivyokuwa, kwa ajili ya utumishi wa Walawi kwa mkono wa Ithamari, mwana wa Haruni, kuhani.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Ifuatayo ni orodha ya vifaa vilivyotumika katika kulijenga hema takatifu, yaani hema la agano. Orodha hii ilitayarishwa na Walawi kwa amri ya Mose, chini ya uongozi wa Ithamari, mwana wa kuhani Aroni.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ifuatayo ni orodha ya vifaa vilivyotumika kwa ajili ya ujenzi wa maskani, maskani ya Ushuhuda, ambavyo vilitayarishwa na Walawi kama alivyoagiza Mose, chini ya usimamizi wa Ithamari, mwana wa kuhani Aroni.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ifuatayo ni orodha ya vifaa vilivyotumika kwa ajili ya ujenzi wa maskani, maskani ya Ushuhuda, ambavyo vilitayarishwa na Walawi kama alivyoagiza Musa, chini ya usimamizi wa Ithamari, mwana wa kuhani Haruni.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Jumla ya vile vyombo vilivyofanywa kwa ajili ya hiyo maskani, hiyo maskani ya ushuhuda ni hii, kama vilivyohesabiwa, kama maagizo ya Musa yalivyokuwa, kwa ajili ya utumishi wa Walawi kwa mkono wa Ithamari, mwana wa Haruni, kuhani.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Ifuatayo ni orodha ya vifaa vilivyotumika katika kulijenga hema takatifu, yaani hema la agano. Orodha hii ilitayarishwa na Walawi kwa amri ya Mose, chini ya uongozi wa Ithamari, mwana wa kuhani Aroni.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Hii ndio hesabu ya mali za kulitengeneza hilo Kao lililokuwa Kao la Ushahidi, nazo zilihesabiwa kwa agizo la Mose; walioifanya kazi hii ndio Walawi, nao waliangaliwa na Itamari, mwana wa mtambikaji Haroni.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Jumla ya vile vyombo vilivyofanywa kwa ajili ya hiyo maskani, hiyo maskani ya ushuhuda ni hii, kama vilivyohesabiwa, kama maagizo ya Musa yalivyokuwa, kwa ajili ya utumishi wa Walawi kwa mkono wa Ithamari, mwana wa Haruni, kuhani.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Hii ndiyo hesabu ya vifaa vilivyotumika katika kujenga hema la kuchunga vile vibao vya agano. Hesabu hii ilitayarishwa na Walawi kwa amri ya Musa, chini ya uongozi wa Itamari mwana wa kuhani Haruni.