Exodus 38:24 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Dhahabu yote waliyomtolea Mwenyezi-Mungu kwa ajili ya ujenzi wa hema takatifu ilikuwa na uzito wa kilo 877 na gramu 300 kulingana na vipimo vya hema takatifu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Jumla ya dhahabu iliyopatikana kutokana na sadaka ya kuinuliwa kwa ajili ya kazi ya mahali patakatifu ilikuwa na uzito wa talanta ishirini na tisa na shekeli mia saba na thelathini (730), kulingana na shekeli ya mahali patakatifu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Dhahabu yote iliyotumiwa kwa ajili ya hiyo kazi, katika kazi hiyo yote ya mahali patakatifu, hiyo dhahabu ya matoleo, ilikuwa ni talanta ishirini na kenda, na shekeli mia saba na thelathini, kwa kadiri ya shekeli ya mahali patakatifu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Dhahabu yote waliyomtolea Mwenyezi-Mungu kwa ajili ya ujenzi wa hema takatifu ilikuwa na uzito wa kilo 877 na gramu 300 kulingana na vipimo vya hema takatifu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Jumla ya dhahabu iliyopatikana kutokana na sadaka ya kuinuliwa kwa ajili ya kazi ya mahali patakatifu ilikuwa na uzito wa talanta 29 na shekeli 730, kulingana na shekeli ya mahali patakatifu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Jumla ya dhahabu iliyopatikana kutokana na sadaka ya kuinuliwa kwa ajili ya kazi ya mahali patakatifu ilikuwa na uzito wa talanta 29 na shekeli 730, kulingana na shekeli ya mahali patakatifu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Dhahabu yote iliyotumiwa kwa ajili ya hiyo kazi, katika kazi hiyo yote ya mahali patakatifu, hiyo dhahabu ya matoleo, ilikuwa ni talanta ishirini na tisa, na shekeli mia saba na thelathini, kwa kadiri ya shekeli ya mahali patakatifu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Dhahabu yote waliyomtolea Mwenyezi-Mungu kwa ajili ya ujenzi wa hema takatifu ilikuwa na uzito wa kilo 877 na gramu 300 kulingana na vipimo vya hema takatifu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Dhahabu zote zilizotumika za kufanya kazi zote za kupatengeneza Patakatifu, zilikuwa dhahabu zilizotolewa kuwa vipaji vya tambiko vya kupitishwa motoni, nazo zilikuwa jumla talanta 29 na sekeli 730, pamoja ndio frasila 80 zikipimwa kwa mizani ya patakatifu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Dhahabu yote iliyotumiwa kwa ajili ya hiyo kazi, katika kazi hiyo yote ya mahali patakatifu, hiyo dhahabu ya matoleo, ilikuwa ni talanta ishirini na kenda, na shekeli mia saba na thelathini, kwa kadiri ya shekeli ya mahali patakatifu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Zahabu yote waliyomutolea Yawe kwa ajili ya kujenga hema takatifu ilikuwa na uzito wa kilo mia nane makumi saba na saba na grama mia tatu kulingana na vipimo vya hema takatifu.