Exodus 38:25 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Fedha waliyochanga hao watu wa jumuiya waliohesabiwa ilikuwa ya uzito wa kilo 3,017 na gramu 750 kulingana na vipimo vya hema takatifu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Fedha iliyopatikana kutokana na jumuiya ya watu waliohesabiwa ilikuwa yenye uzito wa talanta mia moja na shekeli elfu moja mia saba sabini na tano (1,775), kulingana na shekeli ya mahali patakatifu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na fedha ya hao waliohesabiwa, watu wa huo mkutano ilikuwa talanta mia, na shekeli elfu moja na mia saba na sabini na tano kwa kadiri ya shekeli ya mahali patakatifu;
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Fedha waliyochanga hao watu wa jumuiya waliohesabiwa ilikuwa ya uzito wa kilo 3,017 na gramu 750 kulingana na vipimo vya hema takatifu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Fedha iliyopatikana kutokana na jumuiya ya watu waliohesabiwa ilikuwa yenye uzito wa talanta mia moja na shekeli 1,775, kulingana na shekeli ya mahali patakatifu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Fedha iliyopatikana kutokana na jumuiya ya watu waliohesabiwa ilikuwa yenye uzito wa talanta mia moja na shekeli 1,775, kulingana na shekeli ya mahali patakatifu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na fedha ya hao waliohesabiwa, watu wa huo mkutano ilikuwa talanta mia moja, na shekeli elfu moja na mia saba na sabini na tano kwa kadiri ya shekeli ya mahali patakatifu;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Fedha waliyochanga hao watu wa jumuiya waliohesabiwa ilikuwa ya uzito wa kilo 3,017 na gramu 750 kulingana na vipimo vya hema takatifu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nazo fedha zilizotolewa na mkutano kwa kukaguliwa zilikuwa jumla talanta 100 na sekeli 1775, pamoja ndio frasila 244 zikipimwa kwa izani ya Patakatifu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na fedha ya hao waliohesabiwa, watu wa huo mkutano ilikuwa talanta mia, na shekeli elfu moja na mia saba na sabini na tano kwa kadiri ya shekeli ya mahali patakatifu;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Feza waliyochanga hao waliohesabiwa ilikuwa ya uzito wa kilo elfu tatu kumi na saba na grama mia saba makuni tano kulingana na vipimo vya hema takatifu.