Exodus 38:31 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
vikalio vya ua uliolizunguka hema la mkutano na vya lango la ua, na vigingi vyote vya hema takatifu na vya ua.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
vile vitako vya ule ua uliozunguka na vile vya ingilio, na vigingi vyote vya maskani ya Mungu, pamoja na vigingi vya ule ua uliozunguka.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
na matako ya ua kuuzunguka pande zote, na matako ya lango la huo ua, na vigingi vyote vya maskani, na vigingi vyote vya huo ua uliozunguka pande zote.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
vikalio vya ua uliolizunguka hema la mkutano na vya lango la ua, na vigingi vyote vya hema takatifu na vya ua.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
vile vitako vya ule ua uliozunguka na vile vya ingilio, na vigingi vyote vya Maskani pamoja na ule ua uliozunguka.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
vile vitako vya ule ua uliozunguka na vile vya ingilio, na vigingi vyote vya Maskani pamoja na ule ua uliozunguka.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
na vitako vya ua kuuzunguka pande zote, na vitako vya lango la huo ua, na vigingi vyote vya maskani, na vigingi vyote vya huo ua uliozunguka pande zote.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
vikalio vya ua uliolizunguka hema la mkutano na vya lango la ua, na vigingi vyote vya hema takatifu na vya ua.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
nayo miguu ya pande zote za uani na miguu ya langoni penye ua na mambo zote za Kao lenyewe na mambo za pande zote za uani.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
na matako ya ua kuuzunguka pande zote, na matako ya lango la huo ua, na vigingi vyote vya maskani, na vigingi vyote vya huo ua uliozunguka pande zote.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
vikalio vya upango uliolizunguka hema la mukutano na vya mulango wa upango na misumari yote ya hema takatifu na ya upango.