Exodus 38:9 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kisha alilitengenezea ua. Vyandarua vya upande wa kusini wa ua vilikuwa vya kitani safi iliyosokotwa na vyenye urefu wa mita 44;
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kisha akatengeneza ua. Upande wa kusini ulikuwa na urefu wa dhiraa mia moja, na ulikuwa na mapazia ya kitani iliyosokotwa vizuri,
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Naye akafanya ule ua; upande wa kusini kwa kuelekea kusini, chandarua ya ua ilikuwa ya nguo ya kitani nzuri ya kusokotwa, kiasi cha dhiraa mia;
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kisha alilitengenezea ua. Vyandarua vya upande wa kusini wa ua vilikuwa vya kitani safi iliyosokotwa na vyenye urefu wa mita 44;
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kisha akatengeneza ua ambao upande wa kusini ulikuwa na urefu wa dhiraa 100 na ulikuwa na mapazia ya kitani iliyosokotwa vizuri,
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kisha akatengeneza ua. Upande wa kusini ulikuwa na urefu wa dhiraa mia moja, na ulikuwa na mapazia ya kitani iliyosokotwa vizuri,
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Naye akafanya ua; upande wa kusini kwa kuelekea kusini, chandarua cha ua kilikuwa cha nguo ya kitani nzuri ya kusokotwa, kiasi cha dhiraa mia moja;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kisha alilitengenezea ua. Vyandarua vya upande wa kusini wa ua vilikuwa vya kitani safi iliyosokotwa na vyenye urefu wa mita 44;
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kisha akatengeneza ua upande wa kusini ulio wa juani; nguo za ua huo akazitengeneza kwa bafta ngumu, urefu wao ulikuwa mikono mia.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Naye akafanya ule ua; upande wa kusini kwa kuelekea kusini, chandarua ya ua ilikuwa ya nguo ya kitani nzuri ya kusokotwa, kiasi cha dhiraa mia;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kisha akatengenezea hema upango. Mapazia ya upande wa kusini wa upango yalikuwa ya kitani safi iliyosokotwa na yenye urefu wa metre makumi ine na ine;