Exodus 39:1 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kwa kutumia sufu ya rangi ya buluu, ya zambarau na nyekundu walifuma sare za kuvaa wakati wa kuhudumu mahali patakatifu. Walimshonea Aroni mavazi matakatifu kama Mwenyezi-Mungu alivyomwamuru Mose.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kutokana na nyuzi za rangi ya buluu, ya zambarau na nyekundu akatengeneza mavazi yaliyofumwa kwa ajili ya kuhudumu katika mahali patakatifu. Pia akamshonea Haruni mavazi matakatifu, kama Mwenyezi Mungu alivyomwagiza Musa.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na zile nyuzi za rangi ya samawi, na nyuzi za rangi ya zambarau, na nyekundu, wakafanya mavazi yaliyofumwa kwa ustadi sana kwa ajili ya kutumika katika mahali patakatifu, na kuyafanya hayo mavazi matakatifu ya Haruni, vile vile kama Bwana alivyomwagiza Musa.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kwa kutumia sufu ya rangi ya buluu, ya zambarau na nyekundu walifuma sare za kuvaa wakati wa kuhudumu mahali patakatifu. Walimshonea Aroni mavazi matakatifu kama Mwenyezi-Mungu alivyomwamuru Mose.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kutokana na nyuzi za rangi ya buluu, ya zambarau na nyekundu akatengeneza mavazi yaliyofumwa kwa ajili ya kuhudumu katika mahali patakatifu. Pia akamshonea Aroni mavazi matakatifu, kama BWANA alivyomwagiza Mose.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kutokana na nyuzi za rangi ya buluu, ya zambarau na nyekundu akatengeneza mavazi yaliyofumwa kwa ajili ya kuhudumu katika mahali patakatifu. Pia akamshonea Haruni mavazi matakatifu, kama bwana alivyomwagiza Musa.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na zile nyuzi za rangi ya buluu, zambarau na nyekundu, wakafanya mavazi yaliyofumwa kwa ustadi sana kwa ajili ya kutumika katika mahali patakatifu, na kuyatengeneza hayo mavazi matakatifu ya Haruni, vile vile kama BWANA alivyomwagiza Musa.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kwa kutumia sufu ya rangi ya buluu, ya zambarau na nyekundu walifuma sare za kuvaa wakati wa kuhudumu mahali patakatifu. Walimshonea Aroni mavazi matakatifu kama Mwenyezi-Mungu alivyomwamuru Mose.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Zile nguo za kifalme nyeusi na nyekundu walizitumia za kutengeneza mavazi mazuri ya kutumikia Patakatifu, wakayatengeneza hayo mavazi matakatifu ya Haroni, kama Bwana alivyomwagiza Mose.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na zile nyuzi za rangi ya samawi, na nyuzi za rangi ya zambarau, na nyekundu, wakafanya mavazi yaliyofumwa kwa ustadi sana kwa ajili ya kutumika katika mahali patakatifu, na kuyafanya hayo mavazi matakatifu ya Haruni, vile vile kama BWANA alivyomwagiza Musa.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kwa kutumia sufu ya rangi ya samawi, zambarau na nyekundu walifuma nguo za kuvaa wakati wa kutumika katika Pahali Patakatifu. Walimushonea Haruni nguo takatifu kama vile Yawe alivyomwamuru Musa.