Exodus 39:14 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Basi, palikuwa na mawe kumi na mawili yaliyochorwa majina kumi na mawili ya wana wa Israeli. Yalikuwa yamechorwa kama wachoravyo mhuri, kila moja limechorwa jina kuwakilisha makabila kumi na mawili.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kulikuwa na vito kumi na viwili, kimoja kwa kila jina la wana wa Israeli; kila kimoja kilichorwa kama muhuri kwa jina mojawapo la makabila yale kumi na mawili.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na hivyo vito vilikuwa vyaandama majina ya wana wa Israeli, kumi na mawili, sawasawa na majina yao; mfano wa kuchora muhuri, kila moja kwa jina lake, kwa zile kabila kumi na mbili.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Basi, palikuwa na mawe kumi na mawili yaliyochorwa majina kumi na mawili ya wana wa Israeli. Yalikuwa yamechorwa kama wachoravyo mhuri, kila moja limechorwa jina kuwakilisha makabila kumi na mawili.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Palikuwa na vito kumi na viwili, kila kimoja kikiwa na jina mojawapo la wana wa Israeli; kila kito kilichorwa kama muhuri kikiwa na jina mojawapo la yale makabila kumi na mawili.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Palikuwa na vito kumi na viwili, kila kimoja kikiwa na jina mojawapo la wana wa Israeli; kila kimoja kilichorwa kama muhuri kikiwa na jina mojawapo la yale makabila kumi na mawili.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na hivyo vito vilikuwa vyaandama majina ya wana wa Israeli, kumi na mawili, sawasawa na majina yao; mfano wa kuchora mihuri, kila moja kwa jina lake, kwa yale makabila kumi na mawili.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Basi, palikuwa na mawe kumi na mawili yaliyochorwa majina kumi na mawili ya wana wa Israeli. Yalikuwa yamechorwa kama wachoravyo mhuri, kila moja limechorwa jina kuwakilisha makabila kumi na mawili.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Hivyo vito vilikuwa kumi na viwili kwa hesabu ya majina ya wanawe Isiraeli vikiyafuata hayo majina yao, kila kimoja chao kilipata jina lake moja katika hayo mashina kumi na mawili, lilikuwa limechorwa humo, kama kazi ya muhuri ilivyo.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na hivyo vito vilikuwa vyaandama majina ya wana wa Israeli, kumi na mawili, sawasawa na majina yao; mfano wa kuchora muhuri, kila moja kwa jina lake, kwa zile kabila kumi na mbili.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Basi, kulikuwa mawe kumi na mawili yaliyochorwa juu yake majina kumi na mawili ya wana wa Israeli. Yalikuwa yamechorwa kama vile wanavyochora muhuri, juu ya kila moja kulichorwa jina kwa ukumbusho wa makabila kumi na mawili.