Exodus 39:19 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Walitengeneza pete mbili za dhahabu, wakazitia penye ncha mbili za chini upande wa ndani wa kifuko hicho cha kifuani karibu na kizibao.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Akatengeneza pete mbili za dhahabu na kuziunganisha kwenye pembe mbili za chini, upande wa ndani wa kifuko cha kifuani karibu na kizibau.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Nao wakafanya pete mbili za dhahabu, na kuzitia katika ncha mbili za kifuko cha kifuani, katika ukingo wake, ulio upande wa naivera ulio ndani.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Walitengeneza pete mbili za dhahabu, wakazitia penye ncha mbili za chini upande wa ndani wa kifuko hicho cha kifuani karibu na kizibao.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Akatengeneza pete mbili za dhahabu na kuzishikamanisha kwenye pembe mbili za hicho kifuko cha kifuani kwenye ukingo wa ndani karibu na kisibau.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Akatengeneza pete mbili za dhahabu na kuzishikamanisha kwenye pembe mbili za chini, upande wa ndani wa kifuko cha kifuani karibu na kisibau.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Nao wakafanya pete mbili za dhahabu, na kuzitia katika ncha mbili za kifuko cha kifuani, katika ukingo wake, ulio upande wa naivera ulio ndani.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Walitengeneza pete mbili za dhahabu, wakazitia penye ncha mbili za chini upande wa ndani wa kifuko hicho cha kifuani karibu na kizibao.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kisha wakatengeneza tena pete mbili za dhahabu, wakazitia penye zile ncha mbili za chini za kibati cha kifuani katika upindo wake ulioko upande wa ndani uliokielekea kisibau.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Nao wakafanya pete mbili za dhahabu, na kuzitia katika ncha mbili za kifuko cha kifuani, katika ukingo wake, ulio upande wa naivera ulio ndani.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Wakatengeneza pete mbili za zahabu, wakazitia kwenye incha mbili za chini upande wa ndani wa kifuko hicho cha kifua karibu na kizibao.