Exodus 39:30 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kisha walitengeneza pambo la dhahabu safi kwa ajili ya taji takatifu na kuchora juu yake kama wachoravyo mhuri, “Wakfu kwa Mwenyezi-Mungu.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kisha akatengeneza lile bamba, taji takatifu, kwa dhahabu safi na kuchora juu yake maneno haya kama vile muhuri huchorwa: Mtakatifu kwa Mwenyezi Mungu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Nao wakafanya hilo bamba la hiyo taji takatifu la dhahabu safi, na kuandika juu yake andiko, mfano wa kuchorwa kwa muhuri, MTAKATIFU KWA Bwana.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kisha walitengeneza pambo la dhahabu safi kwa ajili ya taji takatifu na kuchora juu yake kama wachoravyo mhuri, “Wakfu kwa Mwenyezi-Mungu.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kisha akatengeneza bamba, taji takatifu, kwa dhahabu safi na kuchora juu yake kama mchoro juu ya muhuri: MTAKATIFU KWA BWANA.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kisha akatengeneza lile bamba, taji takatifu, kwa dhahabu safi na kuchora juu yake maneno haya kama vile muhuri huchorwa: mtakatifu kwa bwana.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Nao wakafanya hilo bamba la hilo taji takatifu la dhahabu safi, na kuandika juu yake andiko, mfano wa kuchorwa kwa mhuri, MTAKATIFU KWA BWANA.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kisha walitengeneza pambo la dhahabu safi kwa ajili ya taji takatifu na kuchora juu yake kama wachoravyo mhuri, “Wakfu kwa Mwenyezi-Mungu.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kisha wakatengeneza kwa dhahabu tupu bamba kuwa taji takatifu ya pajini, wakachora humo machoro yaliyokuwa kama machoro ya muhuri kwamba: Mtakatifu wa Bwana.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Nao wakafanya hilo bamba la hiyo taji takatifu la dhahabu safi, na kuandika juu yake andiko, mfano wa kuchorwa kwa muhuri, MTAKATIFU KWA BWANA.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kisha wakatengeneza pambo la zahabu safi kwa ajili ya taji takatifu na kuchora juu yake kama vile wanavyochora muhuri: Takatifu kwa Yawe.