Exodus 39:5 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mkanda uliofumwa kwa ustadi juu yake ili kuifungia ulikuwa kitu kimoja na kizibao hicho, na ulitengenezwa kwa vitu hivyohivyo: Dhahabu, sufu ya buluu, zambarau na nyekundu, na kitani safi iliyosokotwa, kama Mwenyezi-Mungu alivyomwamuru Mose.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mshipi wa kiunoni uliofumwa kwa ustadi ulifanana nacho: ulikuwa kitu kimoja na hicho kizibau, nao ulitengenezwa kwa dhahabu na nyuzi za rangi ya buluu, za zambarau, na nyekundu na kwa kitani iliyosokotwa vizuri, kama Mwenyezi Mungu alivyomwagiza Musa.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na huo mshipi wa kazi ya werevu, uliokuwa juu yake ili kuifunga mahali pake; ulikuwa wa kitu kimoja, na wa kazi moja na naivera ya dhahabu, na rangi ya samawi, na rangi ya zambarau, na nyekundu, na kitani nzuri ya kusokotwa; vile vile kama Bwana alivyomwagiza Musa.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mkanda uliofumwa kwa ustadi juu yake ili kuifungia ulikuwa kitu kimoja na kizibao hicho, na ulitengenezwa kwa vitu hivyohivyo: dhahabu, sufu ya buluu, zambarau na nyekundu, na kitani safi iliyosokotwa, kama Mwenyezi-Mungu alivyomwamuru Mose.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Mshipi wa kiunoni uliofumwa kwa ustadi ulifanana nacho, ulikuwa kitu kimoja na hicho kisibau, nao ulitengenezwa kwa nyuzi za rangi ya dhahabu, ya buluu, ya zambarau, na nyekundu na kwa kitani iliyosokotwa vizuri, kama BWANA alivyomwagiza Mose.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Mshipi wa kiunoni uliofumwa kwa ustadi ulifanana nacho: ulikuwa kitu kimoja na hicho kisibau, nao ulitengenezwa kwa dhahabu na nyuzi za rangi ya buluu, za zambarau, na nyekundu na kwa kitani iliyosokotwa vizuri, kama bwana alivyomwagiza Musa.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na huo mshipi wa kazi ya werevu, uliokuwa juu yake ili kuifunga mahali pake; ulikuwa wa kitu kimoja, na wa kazi moja na naivera ya dhahabu, na rangi ya buluu, zambarau na nyekundu, na kitani nzuri ya kusokotwa; vile vile kama BWANA alivyomwagiza Musa.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mkanda uliofumwa kwa ustadi juu yake ili kuifungia ulikuwa kitu kimoja na kizibao hicho, na ulitengenezwa kwa vitu hivyohivyo: Dhahabu, sufu ya buluu, zambarau na nyekundu, na kitani safi iliyosokotwa, kama Mwenyezi-Mungu alivyomwamuru Mose.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nayo masombo yake ya kukifunga kifuani pake yalikuwa ya kazi iyo hiyo: yalitengenezwa kwa dhahabu na kwa nguo za kifalme nyeusi na nyekundu na kwa nguo za bafta ngumu, kama Bwana alivyomwagiza Mose.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na huo mshipi wa kazi ya werevu, uliokuwa juu yake ili kuifunga mahali pake; ulikuwa wa kitu kimoja, na wa kazi moja na naivera ya dhahabu, na rangi ya samawi, na rangi ya zambarau, na nyekundu, na kitani nzuri ya kusokotwa; vile vile kama BWANA alivyomwagiza Musa.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mukaba uliofumwa kwa ufundi juu yake kwa kuifunga ulikuwa kitu kimoja na kizibao hicho, na ulitengenezwa kwa vitu hivyohivyo: zahabu, sufu ya samawi, zambarau na nyekundu, na kitani safi iliyosokotwa, kama vile Yawe alivyomwamuru Musa.