Exodus 39:8 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mafundi walitengeneza kifuko cha kifuani kama vile walivyokitengeneza kile kizibao, kwa dhahabu, kwa sufu ya rangi ya buluu, rangi zambarau na nyekundu, na kwa kitani safi iliyosokotwa.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Akatengeneza kifuko cha kifuani, kazi ya fundi stadi. Akakitengeneza kama kile kizibau: cha dhahabu, na nyuzi za rangi ya buluu, za zambarau, na za rangi nyekundu, cha kitani safi iliyosokotwa.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Naye akafanya kile kifuko cha kifuani, kazi ya fundi stadi, kama hiyo kazi ya naivera; ya nyuzi za dhahabu, na za rangi ya samawi, na za rangi ya zambarau, na nyekundu, na kitani nzuri ya kusokotwa.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mafundi walitengeneza kifuko cha kifuani kama vile walivyokitengeneza kile kizibao, kwa dhahabu, kwa sufu ya rangi ya buluu, rangi zambarau na nyekundu, na kwa kitani safi iliyosokotwa.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Akatengeneza kifuko cha kifuani, kazi ya fundi stadi. Akakitengeneza kama kile kisibau: kwa nyuzi za rangi ya dhahabu, ya buluu, ya zambarau, nyekundu na za kitani iliyosokotwa vizuri.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Akafanyiza kifuko cha kifuani, kazi ya fundi stadi. Akakitengeneza kama kile kisibau: cha dhahabu, na nyuzi za rangi ya buluu, za zambarau, na za rangi nyekundu, cha kitani safi iliyosokotwa.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Naye akafanya kile kifuko cha kifuani, kazi ya fundi stadi, kama hiyo kazi ya naivera; ya nyuzi za dhahabu, na za rangi ya buluu, zambarau na nyekundu, na kitani nzuri ya kusokotwa.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mafundi walitengeneza kifuko cha kifuani kama vile walivyokitengeneza kile kizibao, kwa dhahabu, kwa sufu ya rangi ya buluu, rangi zambarau na nyekundu, na kwa kitani safi iliyosokotwa.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kisha wakakitengeneza kibati cha kifuani, nacho kilikuwa kazi ya ufundi wa kweli kama ile kazi ya kisibau, nacho kilitengenezwa kwa dhahabu na kwa nguo za kifalme nyeusi na nyekundu na kwa nguo za bafta ngumu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Naye akafanya kile kifuko cha kifuani, kazi ya fundi stadi, kama hiyo kazi ya naivera; ya nyuzi za dhahabu, na za rangi ya samawi, na za rangi ya zambarau, na nyekundu, na kitani nzuri ya kusokotwa.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Wafundi walitengeneza kifuko cha kifua kama vile walivyotengeneza kile kizibao, kwa zahabu, kwa sufu ya rangi ya samawi, ya zambarau na ya nyekundu, na kwa kitani safi iliyosokotwa.