Exodus 4:10 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Lakini Mose akamwambia Mwenyezi-Mungu, “Ewe Bwana wangu, mimi sina ufasaha wa kuongea tangu zamani; hata baada ya wewe kusema nami mtumishi wako. Ulimi wangu ni mzito.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Musa akamwambia Mwenyezi Mungu, “Ee Bwana, kamwe sijapata kuwa msemaji kwa ufasaha hapo awali, wala tangu ulipoanza kuzungumza na mtumishi wako. Ulimi wangu ni mzito kuzungumza.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Musa akamwambia Bwana Ee Bwana, mimi si msemaji, tokea zamani, wala tokea hapo uliposema na mtumishi wako; maana mimi si mwepesi wa kusema, na ulimi wangu ni mzito.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Lakini Mose akamwambia Mwenyezi-Mungu, “Ewe Bwana wangu, mimi sina ufasaha wa kuongea tangu zamani; hata baada ya wewe kusema nami mtumishi wako. Ulimi wangu ni mzito.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Mose akamwambia BWANA, “Ee Bwana, kamwe sijapata kuwa msemaji kwa ufasaha wakati uliopita wala tangu ulipoanza kuzungumza na mtumishi wako. Ulimi wangu ni mzito kuzungumza.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Musa akamwambia bwana, “Ee Bwana, kamwe sijapata kuwa msemaji kwa ufasaha wakati uliopita wala tangu ulipoanza kuzungumza na mtumishi wako. Ulimi wangu ni mzito kuzungumza.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Musa akamwambia BWANA Ee Bwana, mimi si msemaji, tokea zamani, wala tokea hapo uliposema na mtumishi wako; maana mimi si mwepesi wa kusema, na ulimi wangu ni mzito.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Lakini Mose akamwambia Mwenyezi-Mungu, “Ewe Bwana wangu, mimi sina ufasaha wa kuongea tangu zamani; hata baada ya wewe kusema nami mtumishi wako. Ulimi wangu ni mzito.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini Mose akamwambia Bwana: E Bwana wangu! Mimi si mtu ajuaye kusema tangu kale, wala tangu hapo, ulipoanza kusema na mtumishi wako, kwani kinywa changu ni kigumu, nao ulimu wangu ni mzito.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Musa akamwambia BWANA Ee Bwana, mimi si msemaji, tokea zamani, wala tokea hapo uliposema na mtumishi wako; maana mimi si mwepesi wa kusema, na ulimi wangu ni mzito.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Lakini Musa akamwambia Yawe: “Ewe Bwana wangu, mimi mutumishi wako sina ufundi wa kusema tangu zamani, hata kisha kusema nawe. Ulimi wangu ni muzito.”