Exodus 4:31 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Watu wakaamini. Na waliposikia kwamba Mwenyezi-Mungu amewajia kuwasaidia Waisraeli, na kwamba ameyaona mateso yao, wote wakainamisha vichwa vyao na kumwabudu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
nao wakaamini. Nao waliposikia kuwa Mwenyezi Mungu anajishughulisha nao, na kwamba ameona mateso yao, walisujudu na kuabudu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Watu wakaamini, na waliposikia ya kuwa Bwana amewajilia wana wa Israeli, na ya kuwa ameyaona mateso yao, wakainama vichwa vyao wakasujudu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Watu wakaamini. Na waliposikia kwamba Mwenyezi-Mungu amewajia kuwasaidia Waisraeli, na kwamba ameyaona mateso yao, wote wakainamisha vichwa vyao na kumwabudu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
nao wakaamini. Nao waliposikia kuwa BWANA anajishughulisha nao na kwamba ameona mateso yao, walisujudu na kuabudu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
nao wakaamini. Nao waliposikia kuwa bwana anajishughulisha nao, na kwamba ameona mateso yao, walisujudu na kuabudu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Watu wakaamini, na waliposikia ya kuwa BWANA amewajia wana wa Israeli, na ya kuwa ameyaona mateso yao, wakainamisha vichwa vyao wakasujudu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Watu wakaamini. Na waliposikia kwamba Mwenyezi-Mungu amewajia kuwasaidia Waisraeli, na kwamba ameyaona mateso yao, wote wakainamisha vichwa vyao na kumwabudu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ndipo, watu hao walipoyategemea yale maneno; nao waliposikia, ya kuwa Bwana amewakagua wana wa Isiraeli na kuyatazama mateso yao, wakainama na kumwangukia Mungu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Watu wakaamini, na waliposikia ya kuwa BWANA amewajilia wana wa Israeli, na ya kuwa ameyaona mateso yao, wakainama vichwa vyao wakasujudu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Watu wakaamini. Na waliposikia kwamba Yawe amekuja kuwasaidia Waisraeli na kwamba ameyaona mateso yao, wote wakainamisha vichwa vyao na kumwabudu.