Exodus 4:7 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kisha Mungu akamwambia, “Ingiza tena mkono wako kifuani mwako!” Mose akauingiza mkono wake kifuani. Na alipoutoa nje, kumbe ukarudia hali yake ya kawaida kama ulivyo mwili wake.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mungu akamwambia, “Sasa urudishe tena huo mkono ndani ya joho lako.” Basi Musa akaurudisha mkono wake ndani ya joho lake na alipoutoa, ulikuwa mzima, kama sehemu zingine za mwili wake.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Akasema, Tia mkono wako kifuani mwako tena. Akautia mkono wake kifuani mwake tena, na alipoutoa kifuani mwake, kumbe! Umerudia hali ya mwili wake.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kisha Mungu akamwambia, “Ingiza tena mkono wako kifuani mwako!” Mose akauingiza mkono wake kifuani. Na alipoutoa nje, kumbe ukarudia hali yake ya kawaida kama ulivyo mwili wake.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Mungu akamwambia, “Sasa urudishe tena huo mkono ndani ya joho lako.” Basi Mose akaurudisha mkono wake ndani ya joho lake na alipoutoa, ulikuwa mzima, kama sehemu zingine za mwili wake.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Mungu akamwambia, “Sasa urudishe tena huo mkono ndani ya joho lako.” Basi Musa akaurudisha mkono wake ndani ya joho lake na alipoutoa, ulikuwa mzima, kama sehemu zingine za mwili wake.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Akasema, Tia mkono wako kifuani mwako tena. Akautia mkono wake kifuani mwake tena, na alipoutoa kifuani mwake, kumbe! Umerudia hali ya mwili wake.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kisha Mungu akamwambia, “Ingiza tena mkono wako kifuani mwako!” Mose akauingiza mkono wake kifuani. Na alipoutoa nje, kumbe ukarudia hali yake ya kawaida kama ulivyo mwili wake.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kisha akamwambia: Urudishe mkono wako kifuani pako! Alipourudisha mkono wake kifuani pake na kuutoa kifuani pake akauona, ya kuwa umegeuka tena kuwa kama mwili wake.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Akasema, Tia mkono wako kifuani mwako tena. Akautia mkono wake kifuani mwake tena, na alipoutoa kifuani mwake, kumbe! Umerudia hali ya mwili wake.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kisha Mungu akamwambia: “Ingiza tena mukono wako kwenye kifua chako!” Musa akaingiza mukono wake kwenye kifua. Alipoutoa inje, ukarudilia hali yake ya kawaida kama vile mwili wake unavyokuwa.