Exodus 40:33 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mwishowe Mose akatengeneza ua kulizunguka hema takatifu na madhabahu, na kuweka pazia kwenye lango la ua. Hivyo, Mose akaikamilisha kazi yote.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kisha Musa akatengeneza ua kuizunguka maskani ya Mungu na madhabahu, na pia akaweka pazia kwenye ingilio la huo ua. Hivyo Musa akaikamilisha kazi.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Akausimamisha ukuta wa ua kuizunguka maskani na madhabahu, akalitundika pazia la mlango wa ule ua. Basi Musa akaimaliza hiyo kazi.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mwishowe Mose akatengeneza ua kulizunguka hema takatifu na madhabahu, na kuweka pazia kwenye lango la ua. Hivyo, Mose akaikamilisha kazi yote.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kisha Mose akafanya ua kuizunguka Maskani ya Mungu na madhabahu, pia akaweka pazia kwenye ingilio la huo ua. Hivyo Mose akaikamilisha kazi.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kisha Musa akafanya ua kuizunguka Maskani ya Mungu na madhabahu, pia akaweka pazia kwenye ingilio la huo ua. Hivyo Musa akaikamilisha kazi.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Akausimamisha ukuta wa ua kuizunguka maskani na madhabahu, akalitundika pazia la mlango wa ule ua. Basi Musa akaimaliza hiyo kazi.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mwishowe Mose akatengeneza ua kulizunguka hema takatifu na madhabahu, na kuweka pazia kwenye lango la ua. Hivyo, Mose akaikamilisha kazi yote.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kisha akausimamisha ua wa kulizunguka Kao na meza ya kutambikia, kisha akalitungika pazia langoni kwa ua. Ndivyo, Mose alivyozimaliza hizi kazi.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Akausimamisha ukuta wa ua kuizunguka maskani na madhabahu, akalitundika pazia la mlango wa ule ua. Basi Musa akaimaliza hiyo kazi.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kwa mwisho Musa akatengeneza upango kuzunguka hema takatifu na mazabahu na kuweka pazia kwenye mulango wa upango. Hivyo, Musa akakamilisha kazi yote.