Exodus 5:17 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Lakini Farao akasema, “Wavivu nyinyi; nyinyi ni wavivu, ndio maana mnasema, ‘Tuache twende tukamtambikie Mwenyezi-Mungu’.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Farao akasema, “Ninyi ni wavivu ndiyo sababu mnasema, ‘Turuhusu twende tukamtolee Mwenyezi Mungu dhabihu.’
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Akasema, Wavivu ninyi; wavivu; kwa ajili hii mwasema, Tupe ruhusa twende kumtolea Bwana dhabihu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Lakini Farao akasema, “Wavivu nyinyi; nyinyi ni wavivu, ndio maana mnasema, ‘Tuache twende tukamtambikie Mwenyezi-Mungu’.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Farao akasema, “Ninyi ni wavivu ndiyo sababu mnasema, ‘Turuhusu twende tukamtolee BWANA dhabihu.’
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Farao akasema, “Ninyi ni wavivu ndiyo sababu mnasema, ‘Turuhusu twende tukamtolee bwana dhabihu.’
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Akasema, Wavivu ninyi; wavivu; kwa ajili hii mwasema, Tupe ruhusa twende kumtolea BWANA dhabihu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Lakini Farao akasema, “Wavivu nyinyi; nyinyi ni wavivu, ndio maana mnasema, ‘Tuache twende tukamtambikie Mwenyezi-Mungu’.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini akasema: Ninyi m walegevu, m walegevu kweli. Kawa sababu hii mnasema: Twende, tumtambikie Bwana!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Akasema, Wavivu ninyi; wavivu; kwa ajili hii mwasema, Tupe ruhusa twende kumtolea BWANA dhabihu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Lakini mufalme wa Misri akasema: “Wavivu ninyi! Ninyi ni wavivu, ndiyo maana munasema: ‘Utuache tuende kutoa sadaka kwa Yawe’.