Exodus 5:19 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Basi, hao wasimamizi wa Waisraeli sasa walijiona kuwa wako taabuni, kwani waliambiwa, “Hamtaipunguza kamwe idadi ya matofali ya kila siku.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Wasimamizi wa Waisraeli walitambua kuwa wako taabani walipoambiwa, “Hamtakiwi kupunguza idadi ya matofali mliotakiwa kutengeneza kila siku.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi wanyapara wa wana wa Israeli wakaona ya kwamba wa katika hali mbaya, walipoambiwa, Hamtapunguza hesabu ya matofali yenu hata kidogo; ndizo shughuli zenu za kila siku.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Basi, hao wasimamizi wa Waisraeli sasa walijiona kuwa wako taabuni, kwani waliambiwa, “Hamtaipunguza kamwe idadi ya matofali ya kila siku.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Wasimamizi wa Kiisraeli walitambua kuwa wako taabuni walipoambiwa, “Hamtakiwi kupunguza idadi ya matofali mliotakiwa kutengeneza kila siku.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Wasimamizi wa Kiisraeli walitambua kuwa wako taabani walipoambiwa, “Hamtakiwi kupunguza idadi ya matofali mliotakiwa kutengeneza kila siku.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi wanyapara wa wana wa Israeli wakaona ya kwamba wako katika hali mbaya, walipoambiwa, Hamtapunguza idadi ya matofali yenu hata kidogo; ndizo shughuli zenu za kila siku.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Basi, hao wasimamizi wa Waisraeli sasa walijiona kuwa wako taabuni, kwani waliambiwa, “Hamtaipunguza kamwe idadi ya matofali ya kila siku.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nao waangaliaji wa wana wa Isiraeli wakajiona, ya kuwa wamepatwa na mabaya kwa kuambiwa: Msiipunguze hesabu ya matofali ya siku zote!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi wanyapara wa wana wa Israeli wakaona ya kwamba wa katika hali mbaya, walipoambiwa, Hamtapunguza hesabu ya matofali yenu hata kidogo; ndizo shughuli zenu za kila siku.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Basi, wale wasimamizi wa Waisraeli sasa walijiona kuwa katika taabu, maana waliambiwa: “Hamutapunguza hata kidogo hesabu ya matofali ya kila siku.”