Exodus 5:21 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Basi, wakawaambia Mose na Aroni, “Mwenyezi-Mungu na aone jambo hili na kuwahukumu nyinyi kwa sababu mmetufanya sisi kuwa chukizo kwa Farao na maofisa wake; nyinyi mmewapa sababu ya kutuua.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
wakawaambia Musa na Haruni, “Mwenyezi Mungu na awaangalie awahukumu ninyi! Mmetufanya tuwe chukizo kwa Farao na maafisa wake, nanyi mmeweka upanga mikononi mwao ili kutuua sisi.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
wakawaambia, Bwana awaangalie na kuamua; kwa kuwa mmefanya harufu yetu kuwa chukizo mbele ya Farao, na mbele ya watumishi wake, mkatia upanga mikononi mwao, watuue.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Basi, wakawaambia Mose na Aroni, “Mwenyezi-Mungu na aone jambo hili na kuwahukumu nyinyi kwa sababu mmetufanya sisi kuwa chukizo kwa Farao na maofisa wake; nyinyi mmewapa sababu ya kutuua.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
wakawaambia Mose na Aroni, “BWANA na awaangalie awahukumu ninyi! Mmetufanya tunuke kwa Farao na maafisa wake, nanyi mmeweka upanga mikononi mwao ili kutuua sisi.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
wakawaambia Musa na Haruni, “ bwana na awaangalie awahukumu ninyi! Mmetufanya tunuke kwa Farao na maafisa wake, nanyi mmeweka upanga mikononi mwao ili kutuua sisi.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
wakawaambia, BWANA awaangalie na kuamua; kwa kuwa mmefanya harufu yetu kuwa chukizo mbele ya Farao, na mbele ya watumishi wake, mkatia upanga mikononi mwao, watuue.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Basi, wakawaambia Mose na Aroni, “Mwenyezi-Mungu na aone jambo hili na kuwahukumu nyinyi kwa sababu mmetufanya sisi kuwa chukizo kwa Farao na maofisa wake; nyinyi mmewapa sababu ya kutuua.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ndipo, walipowaambia: Bwana na awatazame ninyi, mlivyo, awapatilize! Kwani mmeufanya mnuko wetu kuwa mbaya puani mwake Farao namo puani mwao watumishi wake, mkawapa panga mikononi mwao, watuue.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
wakawaambia, BWANA awaangalie na kuamua; kwa kuwa mmefanya harufu yetu kuwa chukizo mbele ya Farao, na mbele ya watumishi wake, mkatia upanga mikononi mwao, watuue.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Basi, wakawaambia Musa na Haruni: “Yawe aone jambo hili na kuwahukumu ninyi kwa sababu mumetufanya sisi kuwa chukizo kwa mufalme wa Misri na wakubwa wake. Ninyi mumewapa sababu ya kutuua.”