Exodus 5:3 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mose na Aroni wakamwambia, “Mungu wa Waebrania amekutana nasi. Tunakusihi utuache twende zetu jangwani mwendo wa siku tatu tukamtambikie Mwenyezi-Mungu, Mungu wetu. La sivyo, yeye atatuua kwa maradhi mabaya au vita.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ndipo Musa na Haruni wakasema, “Mungu wa Waebrania amekutana nasi. Sasa turuhusu tuwe na safari ya siku tatu ya jangwani ili tukamtolee Mwenyezi Mungu, Mungu wetu, dhabihu, la sivyo aweza kutupiga sisi kwa tauni au kwa upanga.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Wakasema, Mungu wa Waebrania amekutana nasi; twakuomba, tupe ruhusa twende safari ya siku tatu jangwani, tumtolee dhabihu Bwana, Mungu wetu; asije akatupiga kwa tauni, au kwa upanga.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mose na Aroni wakamwambia, “Mungu wa Waebrania amekutana nasi. Tunakusihi utuache twende zetu jangwani mwendo wa siku tatu tukamtambikie Mwenyezi-Mungu, Mungu wetu. La sivyo, yeye atatuua kwa maradhi mabaya au vita.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ndipo Mose na Aroni wakasema, “Mungu wa Waebrania amekutana nasi. Sasa turuhusu tuwe na safari ya siku tatu ya jangwani ili tukamtolee BWANA Mungu wetu dhabihu, la sivyo aweza kutupiga sisi kwa tauni au kwa upanga.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ndipo Musa na Haruni wakasema, “Mungu wa Waebrania amekutana nasi. Sasa turuhusu tuwe na safari ya siku tatu ya jangwani ili tukamtolee bwana Mwenyezi Mungu wetu dhabihu, la sivyo aweza kutupiga sisi kwa tauni au kwa upanga.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Wakasema, Mungu wa Waebrania amekutana nasi; twakuomba, tupe ruhusa twende safari ya siku tatu jangwani, tumtolee dhabihu BWANA, Mungu wetu; asije akatupiga kwa tauni, au kwa upanga.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mose na Aroni wakamwambia, “Mungu wa Waebrania amekutana nasi. Tunakusihi utuache twende zetu jangwani mwendo wa siku tatu tukamtambikie Mwenyezi-Mungu, Mungu wetu. La sivyo, yeye atatuua kwa maradhi mabaya au vita.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nao wakasema: Mungu wa Waebureo amekutana nasi, kwa hiyo tunataka kwenda nyikani safari ya siku tatu, tumtambikie Bwana Mungu wetu, asitupige kwa magonjwa yauayo wala kwa upanga.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Wakasema, Mungu wa Waebrania amekutana nasi; twakuomba, tupe ruhusa twende safari ya siku tatu jangwani, tumtolee dhabihu BWANA, Mungu wetu; asije akatupiga kwa tauni, au kwa upanga.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Musa na Haruni wakamwambia: “Mungu wa Waebrania amekutana nasi. Tunakusihi utuache tujiendee katika jangwa mwendo wa siku tatu tutoe sadaka kwa Yawe, Mungu wetu. Kama sivyo, yeye atatuua kwa ugonjwa mukali au kwa upanga.”