Exodus 5:7 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“Tangu leo msiwape watu hawa nyasi za kutengenezea matofali kama ilivyo kawaida. Wao wenyewe watakwenda kujitafutia.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Tangu sasa msiwape hawa watu nyasi za kutengenezea matofali; wakusanye nyasi zao wenyewe.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Msiwape watu tena majani ya kufanyia matofali, kama mlivyofanya tangu hapo; na waende wakatafute majani wenyewe.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“Tangu leo msiwape watu hawa nyasi za kutengenezea matofali kama ilivyo kawaida. Wao wenyewe watakwenda kujitafutia.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Tangu sasa msiwape hawa watu nyasi za kutengenezea matofali. Wao wakusanye nyasi zao wenyewe.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Tangu sasa msiwape hawa watu nyasi za kutengenezea matofali. Wao wakusanye nyasi zao wenyewe.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Msiwape watu tena majani ya kufanyia matofali, kama mlivyofanya tangu hapo mwanzo; na waende wakatafute majani wenyewe.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
“Tangu leo msiwape watu hawa nyasi za kutengenezea matofali kama ilivyo kawaida. Wao wenyewe watakwenda kujitafutia.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Watu hawa msiwape tena majani makavu ya kuumbia matofali kama siku zote! Sharti waende wenyewe kujiokotea majani makavu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Msiwape watu tena majani ya kufanyia matofali, kama mlivyofanya tangu hapo; na waende wakatafute majani wenyewe.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
“Tangu leo musiwape watu hawa nyasi za kutengeneza matofali kama vile inavyokuwa kawaida. Wao wenyewe watakwenda kujitafutia.