Exodus 6:12 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Lakini Mose akamwambia Mwenyezi-Mungu, “Tazama, Waisraeli hawanisikilizi mimi, sembuse Farao! Tena mimi ni mtu asiye na ufasaha wa kuongea!”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Lakini Musa akamwambia Mwenyezi Mungu, “Ikiwa Waisraeli hawatanisikiliza, kwa nini yeye Farao anisikilize mimi, ambaye huzungumza kwa kigugumizi?”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Musa akanena mbele ya Bwana, akasema, Tazama, hao wana wa Israeli hawakunisikiza mimi; basi huyo Farao atanisikizaje, mimi niliye na midomo isiyo tohara?
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Lakini Mose akamwambia Mwenyezi-Mungu, “Tazama, Waisraeli hawanisikilizi mimi, sembuse Farao! Tena mimi ni mtu asiye na ufasaha wa kuongea!”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Lakini Mose akamwambia BWANA, “Ikiwa Waisraeli hawatanisikiliza, kwa nini yeye Farao anisikilize mimi, ambaye huzungumza kwa kigugumizi?”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Lakini Musa akamwambia bwana, “Ikiwa Waisraeli hawatanisikiliza, kwa nini yeye Farao anisikilize mimi, ambaye huzungumza kwa kigugumizi?”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Musa akanena mbele za BWANA, akasema, Tazama, hao wana wa Israeli hawakunisikiliza mimi; basi huyo Farao atanisikilizaje, mimi niliye na midomo isiyo tohara?
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Lakini Mose akamwambia Mwenyezi-Mungu, “Tazama, Waisraeli hawanisikilizi mimi, sembuse Farao! Tena mimi ni mtu asiye na ufasaha wa kuongea!”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini Mose akamwambia Bwana waziwazi kwamba: Tazama! Wana wa Isiraeli wasiponisikia, Farao atanisikiaje mimi niliye mwenye midomo isiyofunguliwa kusema vema?
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Musa akanena mbele ya BWANA, akasema, Tazama, hao wana wa Israeli hawakunisikiza mimi; basi huyo Farao atanisikizaje, mimi niliye na midomo isiyo tohara?
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Lakini Musa akamwambia Yawe: “Angalia, Waisraeli hawanisikilizi mimi. Namna gani mufalme wa Misri atanisikia! Tena mimi ni mutu asiyekuwa na ujuzi wa kuongea!”